Habari

MAALI SEIF..Avunja utaratibu wa Itifaki..Aamua kundoka mwisho uwanjani

Kutoka ukurasa wa ‘facebook’ wa Ismail Jussa na watu wengine

Posted: Jumamosi, Aprili 18, 2015 (5:40pm ukt)

KATIBU MKUU wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo alikuwa ni mtu wa mwisho kuondoka uwanjani baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho ulifanyika Jimbo la Kitope, Kaskazini B, Unguja.

Utaratibu huo haukuzoeleka katika kuzingatia itifaki ‘protocol’ kwa shughuli kama mikutano na hafla nyingine zinazojumuisha viongozi wa juu wa serikali na vyama vya siasa.

Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, wiki iliyopita alionekana kuvunja miko ya tabia ya viongozi wa Tanzania, alipokwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam kusikiliza kesi ya kuandamana bila kibali inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wengine 30 wa chama hicho.

Kwa matukio haya mawili ambayo si ya kawaida na hajawahi kufanywa na kiongozi yeyote wa Tanzania, yametoa kielelezo cha waziwazi kuwa Maalim Seif ni kiongozi mwenye imani na mshikamano na wananchi. Yamezidi kupaisha hadhi yake mbele ya macho ya wananchi.

Baada ya mkutano huo kumalizika Maalim Seif, alitangaza kwamba yeye (Seif Sharif Hamad), ataondoka mwisho hadi kuhakikisha kuwa wananchi wote wameondoka na kurudi nyumbani salama.

Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyonukuliwa kwenye ‘facebook’ inaeleza kwamba hotuba na risala za wananchi wa Jimbo la Kitope, zilihanakiza katika Uchaguzi Mkuu na mabadiliko ya wananchi wa jimbo hilo.

Katika risala yao wananchi wa Kitope, walimpa angalizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwamba ajiandae kufunga virago baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu:

Taarifa hiyo inasema: “Tulimwambia Balozi Mkaazi (Seif Ali Iddi) asipambane na bamvua atachanika kifua…wimbi hili ni kubwa…Wazanzibari washaamua na hawazuiliki tena.”

Taarifa inaongeza: “Si Unguja si Pemba…si Kaskazini si Kusini si Mjini si Mashamba…Wazanzibari wameamua hasa kuipa talaka tatu CCM kutokana na udalali waliyoufanya Dodoma.”

Taarifa inasema: “Pamoja na hujuma za viongozi wa CCM na viongozi wa Polisi na mvua kubwa sana iliyokuwa ikinyesha, maelfu ya watu wameshiriki katika mkutano huo wa hadhara kwa moyo mkunjufu na kwa kujiamini.”

Taarifa hiyo ya ‘facebook’ inasema: “Wanachama wapya 287 wamejiunga na CUF wakiwemo wengi waliorudisha kadi za CCM ikiwa ni pamoja na viongozi wa Matawi ya CCM wa jimbo hilo.”

Hadi tunapachika habari hii katika ‘Mzalendo.net…hakuna taarifa zilizoripotiwa za watu kupigwa, kubakwa au kufanyiwa hujuma nyingine na vikundi vya Janjaweed chini ya usimamizi wa CCM na Polisi wa Zanzibar..

Chanzo: Kutoka ‘Facebook page’

Share: