Habari

Maalim Seif: Hatutakubali kuporwa ushindi Zanzibar.

Maalim Seif: Hatutakubali kuporwa ushindi Zanzibar.
NA MWINYI SADALLAH
23rd October 2015

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia cha Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama chake hakitakubali kuporwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kama watakuwa wameshinda.

Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliyofanyika katika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja uzi.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Hassan Nassor Moyo.

Maalim Seif alisema iwapo uchaguzi utakuwa huru na haki, kuna matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi wa asilimia 80 licha ya mizengwe inayoendelea kufanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Alisema kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki, atakuwa wa kwanza kukubali matokeo na kupongeza mshindi kati ya wagombea 14 wanaowania nafasi ya urais.

Lakini alisema iwapo atashinda na ushindi wake kuporwa na kutangazwa mgombea aliyeshindwa, wananchi hawatakubali kurudia makosa kama yaliyotokea miaka ya nyuma visiwani humu. Maalim Seif alisema hayupo tayari kuridhia matokeo yoyote ya ghilba ambayo yatatangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) na kuwataka kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

Share: