Habari

MAANDAMANO YA KUITAKA SMZ IWARUDISHE VIONGOZI WA KIISLAMU ZANZIBAR

Ndugu Wazanzibari kwa heshima kubwa na taadhima tunapenda kutumia fursa tulionayo kikatiba kuwasilisha malalamiko yetu kwa Viongozi wa SMZ kwa njia ya Maandamano.

Maandamano hayo yatafanyika mara tu baada ya sala ya Ijumaa. Maandamano yatakuwa kwa njia ya amani na tusingelipenda kumuona mtu yeyote yule kuchukua silaha ya aina yoyote au hata bakora.

Tunatumia fursa hio ikiwa ni haki yetu kikatiba na pia tunaumwa na matendo wanayofanyiwa Binaadamu wenzetu Wazanzibar wenzetu bila ya kujali dini zao.

Ikumbukwe pia kukaa kimya ni udhaifu na nikuonesha tunaridhia hayo wanayofanyiwa na njia pekee ya kuonesha tunakerwa na hilo ni kuilazimisha serikali iwarudishe haraka Zanzibar na wawashitaki Zanzibar kama vile wanavyoshatakiwa watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa Arusha ambao na wao wanashtakiwa hukohuko Arusha na sio Zanzibar au Dar es salaam.

Maandamano hayo yataanzia misikitini na kuongozwa na masheikh baada ya sala ya Ijumaa na kumalizikia Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko hayo. Maandamano hayatamilizika hadi pale ambapo viongozi husika waliobeba dhima ya kuilinda na kuwalinda Wazanzibar watakapotoa jibu ni lini Viongozi hao waliokamatwa watarudishwa Zanzibar.

Hili ni wajibu wetu sote Kwa kusimama mbele ya muonevu(dhaalimu) kadri ya uwezo wetu na kumsapoti(ALIYEONEWA) iwe kwa uhai,pesa au dua mpaka arudishiwe haki yake . Kuna malipo makubwa katika hili. Mtume(saw) amesema :”Allah humsaidia mja wake madamu tu mja (huyu) humsaidia ndugu yake muislamu”.(MUSLIM).

Pia Mtume(saw) amesema, “Muislamu ni ndugu wa muislamu mwenzake, hivyo asimuonee(asimdhulumu), wala asimkamatishe(asimkabizishe) kwa muonevu(dhaalimu).Yeyote mwenye kumtimizia (kumtatulia) mahitaji ya ndugu yake (muislamu), Allah atamtimizia (atamtatulia) mahitaji yake.
Na yeyote mwenye kumuondolea yasiyomridhisha(matatizo,ugumu,shida nk) ndugu yake (muislamu), Allah atamuondolea yasiyomridhisha(adhabu nk) siku ya kufufuliwa,na yeyote mwenye kumsitiri muislamu,Allah atamsitiri siku ya kufufuliwa.”. Hivyo tuwasaidie na ndugu zetu waislamu waliodhulumiwa kwa kuwalinda wao,haki zao na heshima zao.

Tunashauriana na Wanasheria kama kuna ulazima wa kupata kibali.

Tagsslider
Share: