Habari

MAFUNZO YA (CISM) YAHITIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM.

MAFUNZO YA (CISM) YAHITIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM.

Na Fatma Ally

Mafunzo ya michezo ya masumbwi na mpira wa kikapu ya yaliyoendeshwa na baraza la michezo ya majeshi kimataifa (CISM)yamehitimishwa leo jijini Dar es salaam huku wahitimu wa mafunzo hayo wakitakiwa kutumia weledi.

Mafunzo hayo ambayo jumla ya walimu wa michezo 56 kutoka katika majeshi ya ulinzi na usalama pamoja na raia wamehitimu mafunzo ya siku 10 ya michezo ya ngumi pamoja na mpira wa kikapu.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoendeshwa na wana jeshi kutoka jeshi la Ujerumani kupitia baraza la michezo ya majeshi za kimataifa (Cism) Mwakilishi wa bazara hilo nchini Tanzania, Brigedia Jenerali Suleimani Mzee amewataka wahitimu hao kutumia taaluma hiyo kuebdeleza vipaji vyao pamoja na watu wa chini ambao wanawafundisha.

Kwa upande wake Mkuu wa mafunzo hayo, Kanali Paul Klar amesema amefurahishwa na ukarimu uliyoonyeshwa na wahitimu hao, huku akiahidi kuwa watakuja kutoa mafunzo ya awamu ya pili ambayo yanafanyika mwaka 2019.

Wahitimu hao waatoka katika majeshi ya Wananchi wa Tanzania, Polisi,Zima moto na uokoaji pamoja na raia,ambapo malengo makubwa ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuinua sekta ya michezo katika majeshi pamoja na kukuza mahusiano.

Share: