Habari

Magufuli akiwa Kibandamaiti

Habari waungwana,
Leo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anaendelea na ziara yake visiwani Zanzibar na leo atahutubia Unguja baada ya kutua jana kutoka visiwani Pemba baada ya kuwahutubia wakaazi wa kisiwa hicho. Tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri viwanja vya Demokrasia, Kibandamaiti.
=========

Rais Magufuli: Anaongelea hatua ya Rais Shein kumpa mkono mtu na muhusika kuukataa ‘Kama mtu anakataa mkono wako nawe kataa mkono wake kwa mambo yake, nikuombe nawe uwe unamkatalia mkono wako kufanye mambo yake’ Anamuomba Mungu kumpa walau robo ya moyo wa Shein lakini naye ambae walau robo ya mawazo yake.

Amemwambia ndio maana alivyokuwa Pemba jana, aongeze angalau ukali kidogo.

*Rais Magufuli amesema wanaoshindwa uchaguzi kila mwaka wafikiria kuuza nyanya, kuna watu wengine pia.

*Rais Magufuli amesema hakuna mtu anaekula chama bali chakula, amepeleka makao makuu ya uvuvi Zanzibar ili kupata maendeleo.

*Magufuli: Niwapongeze majeshi yetu ya ulinzi kwa kazi nzuri, kusimamia na kutunza amani, kamanda wenu mkuu niko pamoja na nyinyi.

*Magufuli: Katika maandiko yote mtu anaefarakanisha watu ni shetani, mimi ni Rais wa watanzania wote na nataka umoja.

*Magufuli: Nitatoa ushirikiano mkubwa kwa Dr. Shein ili maendeleo yapatikane, sheria ya gesi ishughulikieni haraka ipitishwe.

*Magufuli: Tunataka maendeleo ya wananchi ndio maana lengo langu kwenu, tushikamane, ni vigumu kupata maendeleo watu wasipoelewana.

==============
Viongozi wote wameshaketi jukwaa kuu akiwemo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein na kwa sasa wanasikiliza utenzi.

Muwakilishi wa wananchi Unguja: Anaeongea kwa sasa ni mwakilishi wa mikoa mitatu ya Unguja na miongoni mwa aliyogusia ni operesheni UKUTA, huduma za kijamii Zanzibar, pongezi kwa Rais Magufuli kuchaguliwa kuongoza nchi na mwisho kumuhakikishia Magufuli kuwa wana shauku ya kumsikiliza na kuyafanyia kazi atakayoyanena.

Anaeongea kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib na anaelezea asili ya neno ‘Kibandamaiti’ kuwa zamani kulikuwa na makaburi mengi na kibanda hivyo watu kukiba jina la Kibandamaiti lakini baadae kiliitwa Kibanda Uhai kwa sababu ya kuwa na watu wengi kuja kwa shughuli za kisiasa, mwisho kinaitwa kiwanja cha demokrasia baada ya shughuli ya demokrasia kukamilika na sasa ni kwa ajili ya shughuli za kisiasa, ziara na watu kupongezana.

Mwisho mkuu wa mkoa anafanya shughuli kuu iliyomleta kutambulisha wageni waliofika kwenye ziara ya leo na wenyeji.

Mwenyekiti wa uchaguzi Zanzibar ameitwa jukwaani baada ya kutajwa jina lake wakati wa utambulisho na waliohudhuria kumtaja kwa nguvu, amesalimiana na Rais Magufuli kisha kuwapa salamu watu waliohudhuria. Baada ya Jecha kutoka ameitwa waziri wa Muungano, January Makamba.

January Makamba: Mheshimiwa Rais ninayo dakika moja, uteuzi wako umenipa mambo mawili, kwanza uenyeji wa Zanzibar na umenipa heshima kubwa sana ya kusimamia tunu ya taifa letu inayotutambulisha, muungano wa Taifa letu. Tatu ziara yako ya kuja Zanzibar. Wakati unatuteua ulisema hutaki kusikia kitu kinaitwa kero za muungano na kazi tumeianza vizuri na muungano wetu utafanikiwa na kudumu.

Nchi yetu ilikuwa kama gari zuri la luxury lakini limetoka barabarani, Rais Magufuli analirudisha barabarani, wengine wameamua kushuka kwenye basi hili.

Mohammed Shein: Anawashukuru wasoma utenzi na Risala, Rais Sheni anasema wananchi wa Tanzania yote wamemchagua Rais kwa kura nyingi sana ambayo ni heshma kwa chama na yeye mwenyewe.

Anasema waliwaomba wananchi wawachague walipokutana Mnazi mmoja, kwa ushindi waiompa Zanzibar ataendelea kuyaenzi mapinduzi ya mwa 1994. Anasema wapo waliokuwa wanajigamba kwenye kampeni za mwaka jana kuwa watawatoa kwenye madaraka lakini wameshindwa wao na kwa kwa utaratibu wa kidemokrasia hawatoitoa kwani watawashinda kila uchaguzi.

Amesema walisema uchaguzi utarudiwa lakini wameshindwa na uchguzi umekwisha na utakaofata ni uchaguzi wa mwaka 2020. Anasema wapo waliothubutu na kusema uchaguzi mwingine utaitishwa na kwenda jumuia ya kimataifa, anahoji jumuiya gani na kwa katiba gani kwani mamlaka ya kuitisha uchaguzi mkuu yamo kwenye katiba ya Zanzibar pekee chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar.

Anamshukuru Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kwa kulipa ufumbuzi wa kudumu suala la mafuta na gesi kwenye awamu iliyopita na anasubiri kutia saini baada ya kupita kwenye bunge la wawakilishi ili mambo yaende kuwa mazuri. Shein anamshukuru Rais Magufuli kwenye suala la uvuvi na anasema nae atafanya jitahada kufanikisha uvuvi Zanzibar ikiwemo viwanda.

JF

Share: