Habari

MAGU- SEFU Idi: Uhuru wa Wazanzibari Unakuja Bila Ya CUF- “Inshallah”

Asalamu aleikhum Warahmatullah Wabarakatuhu ndugu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu. Ama mimi sina budi ila kumshukuru Allah SW kwakunijaalia kufika hapa tena nakuweza kuandika Makala hii ndogo. yenye kichwa cha habari kinachojieleza kwamba. Watanganyika na Dola Yao wasitumie fedha nyingi za Wananchi nakuzunguka zunguka huku na kule kuionyesha dunia na jamii ya Watanganyika na Wazanzibari kwamba CUF ina mgogoro na Maalim Sefu ambae ni Katibu wake kutoka Visiwani amekuwa sasa hatambuliwi na Dola ya  CCM- Tanganyika. KULIKONIIII?

Tunajuwa zamani kwamba Tanganyika ndio Inaitawala Zanzibar kwakutumia Koti la Muungano lilotiwa Viraka viraka vya bandia ili Iimeze Zanzibar. Lengo hilo kila lilipofanywa Zanzibar inajikuta ikifurukuta katika Mdomo wa Mfalme Jeta (Tanganyika) na mihimili yake ya Dola iliojificha kwenye gunia Jeusi. Wazanzibari kimyaaa!  Koti lilijaribiwa Kushonwa upya 2014 na tuliona sintonfahamu ya kutumiliwa Lipumba kuwatowa Wapinzani ndani ya Bunge hilo la Tanganyika; kwa lengo la kuwapa Nafasi akina Mfalme Jeta wajichane kwa kura zao za Wizi. Wazanzibari bado kimyaa na kuwa na msimamo wao ule ule. Walizoea Kuiba na wakawa kama Eliants, hawakuwa na haya kwani hata Maiti, Mahujaji, na Wafu walifika  kupigiwa kura ya Maoni alimuradi tuu  Theluthi 2 ya kura za Wazanzibari zikubali hatakuwa waliopiga ni Watanganyika by status au wafu. Suali jee Katiba ya CCM liipita ? Wazanzibari walizidi kuimarika na kuwa hawayumbi na Msimamo wao wa Zanzibar HURU tena YENYE MAMLAKA KAMILI.

CCM Tanganyika Wakajidanganya kwamba katiba mpya inakuja, na Watanganyika ( Ati) wangetakiwa kupiga kura ya Maoni  kama vile watakavopiga Wazanzibari kuuulizwa juu ya Muungano. (Lakuvunda halina Ubani). Wazanzibari walisubiri kimyaa!  Kilichotushangaza nikuona U-TURN, na Watu kuanza kuogopa vivuli Vyao wenyewe huku wengine wakawa wanageuka nyuma kina  wakilia wanapotizama vivuli vyao akina ( Warioba, Polepole). Wazanzibari kimyaa!… Sio hivo tu bali kuliandaliwa jungu jengine hili lilikuwa lakumtoa Lipumba katika Chama cha CUF wiki chache tuu ya mapambano makali ya Uchaguzi wa 2015- hili lilifanywa ili Wananchi Wakate tamaa na wasipate viti vya kutosha. Hatima Yake wimbi la Mabadiliko halikuja Zanzibar tuu bali hata kwa Watanganyika wenyewe waliweza kuiyangusha CCM- Mpate mpate na mihimili ya Dola iliotumika kuiokoa CCM Tanganyika. Wazanzibari wakaipa CCm suprised ya Miaka 15 ya wizi wao wa kura.

Yote hayo yalipofeli ndipo Tanganyika amejitokeza akiwa hakuvaa koti la Muungano na kutumia mihimili yake ya Dola ambayo haihusiki hata kidogo kujihusisha na Vyama vya Siasa au migogoro ya ndani ya Vyama. Ukikataa ya Mussa Utaona ya Firauni… Miaka 2 hii Wazanzibari tumeweza kuona mambo mengi na kuwa na ufahamu mzima juu ya ndugu zetu hawa wa Damu. (KUPE). Mfano Mihimili ya Dola inayotumika kimacho macho kuihujumu Zanzibar na Wazanzibari ni:

  1. Mahakama kuu
  2. Msajili wa vyama
  3. Bunge lake.
  4. Raia wake halali
  5. Na Jeshi lake

Hakuna mtoto mdogo asiejuwa kwamba Muungano wa Zanzibar na Tanganyika Hauna uhalali wowote ule. Na hii ndio sababu moja kubwa iliompelekea JAKAYA KIWETE na Timu yake ya Wakoloni Weusi kutumia Billioni ya fedha Kutaka kuandika KATIBA MPYA; ambayo njama yake ilikuwa nikuiuwa ile Katiba ya Wazanzibari.

Hivo basi uhalali wa national party such as CHADEMA, CUF, CCM, DP na utitiri mwengine wa vyama ulioko nyuma ya vyama hivi vikuu pia nao hauna uhalali wowote ule. Na Ndio maana katika chaguzi zoote zinazofanyika Zanzibar hakuna Chama hata kilichowahi kushinda hata Uwakilishi wa viti zaidi ya 5. Hata hichi Chama chenu cha Catholics Christian Crusaid (CCM) basi kama hakijabebwa na Dola na Vibaraka wao wenye asili ya Bara kutoka ZEC; basi kisingeweza kushinda zaidi ya viti 5. Ushahidi huo Umeonekana wazi siku ile ya tarehe 20 March 2016: CCM Tanganyika Walipowalazimisha Vibaraka Wao akina Vuia na Jecha, Sefu Iddi kufuta Uchaguzi huru na halali ambao Wazanzibari Walimpa ushindi Maalim Sefu na CUF.

Nikisema hivo ninamaana kwamba Wazanzibari wanaelewa kwamba Mihimili hii 5 ya Vyombo vya Dola ya Tanganyika, yote inatawaliwa na Watanganyika Wenyewe tena wote ni Wakristo. Na Hawa Ndio Maaduwi wakubwa wa  jamii ya Waislamu wa Zanzibar na hata wa Tanganyika. Hakuna  asijuwa kwamba Mihimili hii 5 ya Dola iko chini ya Serikali ya TAnganyika na sio Muungano kwani Muungano wenyewe Haupo, kwasababu Muungano unakuwa wa vitu viwili au zaidi ya viwili. Na vyombo hivi vya dola kama vingekuwa ni vya mUungano ndani yake Wangekuweko Wazanzibari au Watu wa Dini na rangi tofauti. Lakini  Leo Kuna kitu kimoja, chenye watu wenye madhehebu ya dini moja na itikadi moja na rangi moja ambacho kinatawala  kundi jengine nje ya Mipaka yao na kutunga sheria na kuamua maamuzi haramu ya kidhalimu, ukesha ukasema ni chombo cha Muungano.

Nataka kuwakumbusha Watawala kwamba unapomlazimisha Ngombe kunywa maji kwa nguvu basi huwenda ngombe huyo akakugeukia wewe mwenyewe na ukajuta.  Tafakarini kabla hamujatusukuma kabisa katika ukuta, Tanganyika kuna Wazanzibari au Watanganyika ambao wana ndoto yakuiona Tanganyika yao imezaliwa na kuwa na Identity yao kama Watanganyika na halafu wakawa Watanzania. Mutakapoamuwa kutengeneza Mgogoro na machafuko Zanzibar. Mujuwe na nyinyi Huko Tanganyika hamuko Salama.

Msukumo wenu munao wasukuma Wananchi wa Zanzibar kwakuwaona ni kidogo na nyinyi ni Wengi unaweza kuja ku-suprised. Mumeshindwa na njia zote za dhulma na sasa mumeona ni bora  kuwapachika  walafi 3 wenye asili ya Pemba ambo hata katika jamii hawakubaliki.  Jibu letu Wazanzibari tunasema kwamba. Sio CCM wala CUF au hata ASP ndio itakayotupatia UHURU wetu tulioporwa na Watanganyika April 1964.

Sio Chadema wala  CCM au CUF ndio itaimarisha Umoja  na Udugu wa Wazanzibari uliokuwepo asili na jadi za mababu zetu. Kwani hakuna asiejuwa kwamba Umoja wetu na Utamaduni wetu ndio Mwiba mkubwa uliowapelekea Julias Nyerere na kundi lake kutamani kuimeza Zanzibar. Mihimili 5 hii naifanye kazi zisizo wahusu kushuhulikia Siasa za Zanzibar na kuendelea kuhujumu Ndoto yetu ya Mamlaka kamili. REVOLT, REVOLT, REVOLT ambayo imejengwa ndani ya MOYO WETU ndio utakaotupatia Uhuru wetu na kama vile

NATIONALITY:

MORALITY.

SOLIDARITY.
IDENTITY:

Wazanzibari Shime jipangeni Imara, Kike Kiume, Mkubwa Mdogo. Mzee kijana. Siku ikifika tukawa Tumeshaegemezwa Ukutani. Nationali, Morality, Solidarity na Identity ndio Itakuwa Silaha yetu kubwa Kuiondowa CCM madarakani. Kwa Nguvu. Siku hio itafika na Inshallah Dhulma haitodumu

Wabilahi Taufiq

Share: