Habari

Magufuli akabidhiwa orodha ya wafanyakazi wa BOT

Orodha ya wafanyakazi wa Banki Kuu ya Tanzania imeshakamilika na tayari imeshakabidhiwa kwa Rais John Pombe Magufuli tayari kuitumbua au kuiwekea kufuli zaidi.

Waajiriwa wa BOT waliotajwa katika orodha hiyo ni kama ifuatavyo:
Pamela Lowasa mtoto wa Edward Lowasa
Filbert Sumaye mtoto wa Frederick Sumaye
Zakaria Kawawa mtoto wa Rashid Kawawa

Huriet Lumbanga mtoto wa Katibu mkuu Kiongozi Marten Lumbanga awamu ya tatu
Salama Ali Hassan Mwinyi mtoto wa Mzee Ruhsa
Rachel Muganda mtoto wa aliekuwa balozi awamu ya nne Alenxender Lumbanga
Salma Omar Mahita Mtoto wa Omar Mahita kamanda wa polisi.

Justin Mungai mtoto wa Aliekuwa waziri wa Elimu Joseph Mungai
Keneth Nchimbi mtoto w aka jeshi la Polisi
Blasia William Mkapa Mtoto wa Rais Benjamin Mkapa
Violet Phillemon Luhajo mtoto wa aliekuwa katibu mkuu kiongozi Phillemon Luhajo.

Liku Kamba mtoto wa Kada wa CCM Kate Kamba
Thomas Mongela mtoto wa kada mashuhuri CCM alieshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo ubunge Getrude Mongela
Jabir Abdala Kigoda mtoto wa Marehem Abdalla Kigoda waziri wa Biashara na Viwanda

Rais Magufuli aliitaka orodha hiyo alipofanya ziara ya kushtukizia BOT na kuamuru kupewa orodha ya wafanyakazi wa taasisi hiyo ambayo amesema idadi ya wafanyakazi haiendani na ukubwa wa taasisi hiyo yenye waajiriwa 1391 ambao wengi wao hawajulikani kazi zao.

Hata hivyo Taasisi hiyo ya Muungano imekosekana jina la kigogo wa kiongozi yoyote kutoka CCM Zanzibar.

(Nipashe)

Share: