Habari

Magufuli sasa wameandika wasifu wa marehemu (obituary) kwa sera ya mambo ya nje

Magufuli sasa wameandika wasifu wa marehemu (obituary) kwa sera ya mambo ya nje tuliyorithi kutoka kwa Mwalimu.

Imeandikwa na Tundu Lissu

Tuliunga mkono harakati za ukombozi kila mahali palipokuwa na uonevu na ukandamizaji wa kitaifa.

Ndio maana tulikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kuvunja uhusiano na Israel mwaka 1973 baada ya Vita ya Yom Kippur.

Ndio maana sio tu tuliitambua PLO kama mwakilishi halali wa wananchi wa Palestine, bali pia tuliwaruhusu PLO kufungua ubalozi wao Tanzania, licha ya kwamba nchi yao bado inakaliwa kimabavu na Mazayuni.

Sio tu tuliitambua POLISARIO kama mwakilishi halali wa wananchi wa Sahara Magharibi, bali pia tuliwaruhusu POLISARIO kufungua ubalozi wao Tanzania, licha ya kwamba nchi yao bado inakaliwa kimabavu na Morocco.

Sasa tumekuwa kama malaya: kila anayetupa au kuahidi kutupa msaada anapiga tu.

Wale wa Kusini mwa Afrika tuliowasaidia kupata uhuru wao bado wanajitambua. Afrika Kusini imemwita Balozi wake Israel kuonyesha kutokukubaliana na mauaji ya waPalestina Gaza.

Sisi tumeenda kubariki mauaji hayo kwa Balozi wetu kwenda Jerusalem kusherehekea ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Halafu hakuna mjadala wowote, hata Chuo Kikuu, juu ya suala hili.

Fb

Share: