Habari

MAHAKAMA YA RUFAA YATOA UAMUZI WA KUTUPILIA MBALI MAOMBI YA LIPUMBA NA WENZAKE KUHUSU RUZUKU YA CUF:

JOPO LA MAJAJI WATATU WA MAHAKAMA YA RUFAA LATOA UAMUZI WA KUTUPILIA MBALI MAOMBI YA LIPUMBA NA WENZAKE KUHUSU RUZUKU YA CUF:

THE CIVIC UNITED FRONT
[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI:

TAREHE 24 DECEMBER, 2018

MAHAKAMA YA RUFAA MBELE YA JOPO LA MAJAJI WATATU MHE. JAJI MUSSA KIPENKA, MHE. JAJI MZIRAY E. M. S. NA MHE. JAJI NDIKA LEO TAREHE 24/12/2018 Imetupilia mbali na kuamuru kulipwa kwa gharama za kesi/shauri la maombi ya marejeo/rufaa lililofunguliwa Mahakamani hapo na washirika wenzake Lipumba kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu kuzuia Ruzuku ya CUF kupewa Lipumba na genge lake mpaka hapo kesi ya msingi namba 68/2017 itakapotolewa uamuzi.

Akisoma maamuzi haya Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa mbele ya Wakili wa Lipumba Mashaka Ngole na Wakili wa Serikali Rehema Mtuliya, alieleza kuwa;
“…Maombi hayo yamekosa sifa kisheria na hivyo Mahakama kukubaliana na hoja za msingi za Pingamizi la awali liliwekwa na Wasomi Mawakili Daimu Halfani na Juma Nassoro walioiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF katika shauri hilo… na hivyo Mahakama imeyaondoa maombi hayo kwa gharama (Struck Out with Cost)…”

Awali Jopo hilo na Majaji watatu liliketi Tarehe 30/10/2018 na kusikiliza Shauri hilo No. 343/01/2018 lililofunguliwa na Peter Michael Malebo, Thomas Malima na wenzao 7 wajumbe wa Bodi ‘FEKI’ ya Lipumba inayotambuliwa na RITA dhidi ya Bodi halali ya Wadhamini ya CUF inayoongozwa na Katibu wake Joran Lwehabura Bashange, Msajili wa Vyama vya siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Lipumba na Wajumbe wake wa bodi FEKI wanaiomba Mahakama ya Rufaa itengue AMRI ya zuio la kutolewa kwa Ruzuku ya CUF kwenda kwa Lipumba na genge lake kutokana na Amri ya kuzuiwa kutolewa ruzuku hiyo na Mahakama Kuu mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera Tarehe 29/5/2018 katika shauri Namba 80/2017.

Mahakama Kuu ilikubali maombi na kutoa AMRI ya kuzuia Ruzuku ya CUF kutolewa kutokana na shauri lililofunguliwa Mahakamani October, 2017 na THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-CHAMA CHA WANANCHI]- CHINI YA KATIBU WAKE MHE JORAN BASHANGE DHIDI YA THE REGISTRAR OF POLITICAL PARTIES AND THE HONOURABLE ATTORNEY GENERAL.

MAARIFA (BACKGROUND KNOWLEDGE):

Wasomi Mawakili Juma Nassoro na Daimu Halfani kwa pamoja na kwa umahiri mkubwa waliwasilisha hoja za pingamizi (Preliminary Objections) zilizosheheni (Authorities) maamuzi mbalimbali ya Mahakama Kuu za Tanzania, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki. Kwa kueleza kuwa Moja;
Maamuzi yaliyotolewa yalikuwa ni “Interlocutory Order/Decision” chini ya kifungu cha [Section 5(2) (d) Appellate Jurisdiction Act Cap 141 RE 2002 as amended by Act No. 25/2002] ambacho kisheria kinakataza kukatia rufaa au kuombewa kufanyiwa marejeo (Revision) na mahakama ya rufaa.

5(2)(d) “no appeal or application for revision shall lie against or
be Act No.25 of made in respect of any preliminary or interlocutory decision or order of the High Court unless such decision or order has the effect of finally determining the criminal charge or suit”

Pili, maombi yao yameacha kuambatisha Nyaraka muhimu sana kwa mujibu wa sheria na;

Tatu, Utaratibu wa kisheria walipaswa kupeleka maombi kwa Mahakama/Jaji aliyetoa maamuzi hayo kumuomba kuiondoa (discharge), badilisha (varied) au kuweka pendeni (set aside) chini ya [Order XXXVII rule 5 of the Civil Procedure Code, Cap 33 RE 2002] provides, that;

“Any order for an injunction may be discharged, varied, or set aside by the court on application made thereto by any party dissatisfied with such order.”
Na siyo kwenda mahakama ya juu kwa rufaa (appeal) au marejeo (revision).

Kwa upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwakilishwa na Wasomi Mawakili David Kakwaya na Rehema Mtuliya ambao kwa pamoja waliunga mkono hoja za Wasomi Mawakili Juma Nassoro na Daimu Halfani kuiomba Mahakama ya Rufaa itupilie mbali shauri hilo lililofunguliwa na Lipumba na genge lake kwani kwa Nyaraka za hukumu na maamuzi mbalimbali zilizowasilishwa na Wasomi Mawakili wa CUF wanaoiwakilisha Bodi ya Wadhamini, maombi ya Lipumba na genge lake yamekosa sifa kisheria.

kwa upande wa Lipumba na genge lake waliwakilishwa na Wakili Mashaka Ngole na alipotakiwa kujibu hoja zilizowasilishwa alikiri kuwa alikosea kisheria kuwasilisha shauri hilo mahakamani (He concede that, The Application was defective) na kukubaliana na hoja za awali za mapingamizi zilizowekwa na Wasomi Mawakili Juma Nassoro na Daimu Halfani.

HATA HIVYO, akaiomba Mahakama iliangalie shauri hilo kwa “JICHO LA HURUMA KWANI WATEJA WAKE WAMEATHIRIKA NA MAAMUZI YA KUZUIWA RUZUKU NA HIVYO WANAKABILIWA NA HALI MBAYA KIUCHUMI…” (Njaa imetamalaki na kutuwama) jambo linalowakwamisha kutekeleza majukumu yao. Akaiomba Mahakama ya Rufaa iendelee kusikiliza maombi ya marejeo (REVISION) yakiyowasilishwa mbele yake.

Kama kawaida Mashaka Ngole alikuwa na wakati mgumu alipotakiwa na Mahakama kufafanua hoja yake ya kutaka kuendelea kusikiliza shauri ambalo kimsingi halipo mahakamani ni kama kusema.. “The Court cannot move on due to the incompetency of the Application..”

UAMUZI HUU WA LEO unatoa fursa sasa ya Mahakama Kuu kuendelea na kutoa uamuzi wake katika shauri la msingi na. 68/2017 lililofunguliwa na CUF kuitaka mahakama itoe amri kwa Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi kupeleka fedha za ruzuku ya CUF kwa wahusika sahihi na kuingizwa katika akaunti ya benki sahihi iliyoidhinishwa na THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) Chini Ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-CHAMA CHA WANANCHI] KINAWATAKIA WATANZANIA WOTE KRISMAS NJEMA NA KHERI YA MWAKA MPYA 2019 TUKIKUMBUKA KUANZA NA UTEKELEZAJI WA AZIMIO LA ZANZIBAR.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa;

SALIM BIMANI
MKURUGENZI- HABARI
+255 777414112 / +255 655314112

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
maharagande@gmail.com
+255 715062577 / +255 767062577

Share: