Habari

Makame Mbarawa cheo kisikukoseshe adabu.

Kwa masikitiko makubwa sana nimeisikia kauli ya muungwana huyu, nilikuwa katika mapumziko ya muda mrefu kwa sababu afya yangu haikuwa nzuri kwa muda sasa,lakini baada ya kuyapitia maneno ya Makame Mbarawa aliyoyatoa bungeni kumjibu mbunge bi Saada Mkuya,imenibidi nimeze vidonge vyangu vya jioni upesi, baada ya kupata nafuu, sasa naomba kumjibu Makame Mbarawa.

Lugha uliyotumia Makame Mbarawa haikuwa na ulazima hata kidogo,wewe kama kiongozi ungeliweza kumjibu bi Saada Mkuya bila kuwatukana wazee wa wenzio na watu usiowajua, iwe wanakaa vijijini pemba au katika mabaraza ya hapa visiwani,iwe darajani au daraja bovu,wewe kama kiongozi wa watu wote, hukutakiwa kuwabagua watu wako au wa taifa lilikokupa uongozi, hata kama wanaishi chini ya madaraja kwa ukosefu wa pa kuishi{home less}seuze katika vibanda vyao vya makuti au makopo.

Mimi nitakuazima lugha hii ambayo ungeliweza kuitumia kumjibu Bi Saada Mkuya bila kumtusi mtu,hii ni lugha ya kisiasa na kidiplomasia, ambayo kama ungeliitumia,ungeliweza kumfurashisha Bwana wako uliyemkusudia kumfurahisha yaani Rais wa Tanganyika,……..

 

“” Mheshiwa Saada, sisi tunajivunia Tanzania yetu kwa umoja wetu,udugu wetu na muungano wetu,kila mtanzania ana haki kuishi na kufanya kazi popote katika taifa hili,iwe anatoka katika kisiwa cha  Ukerewe,au cha Pemba, atoke Usukumani au Utumbatuni, sote ni raia wa nchi hii,ubaguzi wowote ni mwiko, sio wa chama chetu tu, bali wa taifa letu kwa ujumla, sasa kuwaajiri wazanzibari watupu katika shirika lolote la umma,hilo sio tu ni kosa,bali pia ni kuwadhulumu walipa kodi wa nchi hii, ambao hawachangii maendeleo ya nchi kwa kutarajia malipo kwa kabila/makabila fulani tu, au watu wa maeneo tutakayo chagua sisi viongozi,Ujamaa bado ni siasa safi ya nchi hii, japokuwa tunajaribu ubepari wa hapa na pale,huo utatushinda ndio maana kila tajiri ni fisadi””

 

UNAONA hii ni lugha ya kisiasa tu, haina maana yoyote kwa Wazanzibari halisi wenye uchungu na ardhi yao, watu kama nyie mnaoumiwa ili sisi tuendelee kutawaliwa, mnaweza kusema chochote,muhimu kwenu ni vyeo tu,sasa hakukuwa na ulazima kuonyesha elimu yako duni, kwa wazee na ndugu zetu ambao hawakufanya kosa lolote kwako, zaidi ya kukunyima kura kihalali na hiyo ni haki yao.wewe sio wa kwanza kunyimwa kura muulize rais wa mabavu wa Zanzibar wa sasa wapi aliwahi kuchaguliwa huko nyuma {Pemba).

Mnaweka chuki zenu vifuani bure,mnakimbilia Tangayika kwa mkoloni mara tu mnapokataliwa makwenu,mimi wala sitosema kuwa nyie sio Wazanzibari kosa hilo silifanyi,kwa sababu najua nyie ni Wazanzibari halisi na halali kama nilivyo mimi,tofauti yangu mimi na nyie ni “USALITI TU”

 

Mimi niko tayari tuwe masikini zaidi ya hapa, kama kuma umasikini zaidi ya huu,lakini tuwe HURU, huna la kunidanganya kuhusu muungano wala Tanzania, huu ni Upumbavu mtupu,sisi ni visiwa huru tulikuwa na bado tunao uwezo wa kurudi tuliko toka,tatizo ni watu kama wewe Makame Mbarawa,manaokotwa nje ili mje mrudi Tanganyika, baadae mkabidhiwe Zanzibar kwa manufaa ya nani?

Mnawaona wazee wenu wa vijini pemba kuwa ni wapumbavu pamoja na wale wa Darajani,kumbe wapumbavu wengi wako katika bunge la Tanganyika wanauza VISIWA VYAO kwa vijisenti viwili vitatu,njaa zenu ndio mauti yetu.

Hukunipa sababu hata moja ya kukuheshimu,warka huu mfupi narudisha salaamu tu, wahenga walisema usikaange mbuyu ukawaachia vibogoyo kumun’gunya,ukabaki kinywa wazi na meno lukuki.

 

Cheo utapata kama ulivyoahidiwa,punguza matusi kwa watu wako kwa sasa.jiheshimu uheshimiwe usitarajie mvua jangwani wakati mwitu unaujua.

 

Niasalimie wasaliti wote wenzio, hapo bungeni tafadhali.

 

Zanzibar.

 

Share: