Habari

Malengo ya Mapinduzi yamefikiwa?

Tunafikia kelele cha maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 tukiwa kwenye mitazamo tofauti.

Nimepitia na kukusanya sababu kuu kama zinavyoelezwa kuwa ndio zilikuwa hoja za msingi kufanya mapinduzi yale. Nikawaida kila penye mnyukano wa kisiasa kila mwenye fikra hupenyeza lake.

Nikubaliane na hoja kuwa Mapinduzi ya Zanzibar 1964 yalikuwa ‘complex’ kwa wachambuzi lakini yalikuwa dhahir kama sie wenye upeo mwembamba.

Afro-shirazi Party ilikuwa na malengo yake na Umma Party pia ilikuwa na malengo yake. ASP ikichochewa na Tanganyika kwa dhana ya Uafrika wakati Umma Party wakichochewa na Ukominist. Ideology mbili tofauti. Tukiachia makundi mengine yaliyojipenyeza kutoa mustakbali wa Zanzibar.

Hivyo nimepata sababu kuu zifuatazo kuwa ndio kichocheo cha Mapinduzi.
1) kuondoa utawala wa Kifalme na kuleta utawala wa Kirais
2) kuleta ukombozi kamili ili kuwa huru na kujitawala wenyewe
3) kuondosha ubaguzi na kuleta usawa
4) kutowa elimu kwa usawa na watu wote
5) kutowa matibabu bila ya kulipia
6) kuifanya ardhi kumilikiwa na watu wote

Tunapaswa kuyatathmini kwa uwazi na sio jumla jumla mambo hayo 6 kuona ni kwa kiasi gani miaka hii 54 sababu za mapinduzi zimefanikiwa.

1. Kuondoka kwa utawala wa Kifalme kulipelekea kwa muda wa miaka 20 baadae Zanzibar hakuna uchaguzi. Sio wa Rais wala Wawakilishi. Miaka 34 iliyofuata tumeshuhudia dhahma kubwa kadri unapofika wakati wa uchaguzi. Huku kukiwa na imani ya mshindi hupinduliwa. Juu ya yote nikuwa Rais wa Zanzibar huletwa kutoka Tanganyika.

2. Kuwa huru na kujitawala, hili ndio eneo ambalo limefeli kabisa. Zanzibar iko chini ya mkoloni miezi 3 baada ya mapinduzi. Kuanzia hapo Zanzibar haikuwa na mamlaka tena, Rais wa Zanzibar amekuwa ‘mavi’ tu kwa mkoloni Tanganyika. Wako wanaoamini kifo cha Karume ni mkoloni aliyepanga. Kumuondoa Rais Aboud Jumbe, ni mkoloni, hadi leo hii. Hivyo Zanzibar imerudi kwenye kutaliwa baada ya mapinduzi.

3. Ubaguzi na usawa. Pia hili nalo limerudi nyuma. Wachache ndio wanaojijengea himaya. Wako wanaohodhi haki za watu bila huruma.

3. Elimu, licha ya serikali kujenga skuli nyingi ukilinganisha na kabla ya mapinduzi, hazikidhi haja ya maendeleo ya elimu. Kabla ya mapinduzi Zanzibar haikuwa na shida ya walimu. Sasa hivi Zanzibar inasaidiwa walimu kutoka Nigeria. Kabla ya mapinduzi Zanzibar haikuwa na shida ya vitabu sasa hivi hadi isaidiwe. Mwisho education quality ilikuwa nzuri kuliko sasa hivi.

5. Matibabu bila malipo, ukilinganisha kabla ya mapinduzi pamoja na matibabu ya kulipia yalikuwa yakikidhi sifa ya kuitwa matibabu. Sasa hivi watu wanalipia hawapati ubora wa matibabu. Nimeshuhudia kitanda kinalazwa wagonjwa 3. Ikiwa Sayyid Abdallah Khalifa alikufa Mnazimmoja leo Dr Ali Mohamed Shein kila mwaka anasafiri ya kwenda London checkup tu, Balozi Seif Ali Idd anasafiri ya kwenda Cuba kutibiwa kila muda fulani. Husikii viongozi wa Zanzibar kufia Mnazimmoja, kwa karibu ni Muhimbili.

6. Ardhi, ikiwa serikali leo hii inasema ina mashamba yake au ardhi ni mali ya serikali ni wananchi gani waliofaidika na ardhi baada ya mapinduzi. Hata mimi banayangu anawapa watu sehemu za kulima ikiwa ndio kama hivyo serikali inavyosema imewapa wananchi eka 3. Tukiangalia upande mwengine wananchi wangapi sasa hivi wanashida ya ardhi na hiyo mgogoro wa Ardhi kila siku unakwenda kusuluhishwa inatokana na nini.

Tuendelee kufanya tathmini ya kiuhalisia na sio ushabiki wa kisiasa. Dhamira ya mapinduzi isimamiwe na itekelezwe kwa mujibu wa Gharama za mapinduzi.

Mapinduzi yametugharimu kiasi kikubwa kuwa hadi tumepoteza utambulisho wetu

Share: