Habari

Mama, mwana wauawa kinyama

May 23, 2018

NA ASYA HASSAN

WATU wawili ambao ni mama na mtoto wake, wameuawa kikatili na watu wasiojulikana katika kijiji cha Jendele Guruweni Wilaya ya Kati Unguja.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia jana baada ya mume wa marehemu kufika nyumbani kwake asubuhi na kumuona mkewe na mtoto wake wakiwa wamefariki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan Suleiman, alisibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni Patima Abdalla Makame (27) anaesadikiwa kupigwa na kitu cha ncha kali mfano wa shoka eneo la usoni na mtoto Haji Ismail Haroun, mwenye umri wa miezi mitano, ambae alinyongwa.

“Huyu mume anaitwa Ismail Haroun Mateo (45), ana wake wawili ambapo mke mkubwa anaishi Umbuji ndio alikolala usiku na mke mdogo anaishi Jendele, ilipofika asubuhi saa 1:30 mume alikwenda kwa mke mdogo alipofika aliwakuta wameshafariki” alisema.

Zanzibarleo

Share: