Habari

Mambo 3 yamkimbiza Lowasa CDM: Jee kuna hasara au Faida kwa Upinzani?

Lowassa ni mwana Siasa mkongwe sana wa CCM ambae ameshikilia nafasi nyingi kubwa kubwa ndani ya CCM. Kuondoka kwake CCM kukimbilia Chadema nikutaka kukitia adabu Chama cha CCM kwakuto kumteua kuwa mgombea uraisi wa kwa ticket ya Catholics Christian Movement ( CCM). Na alipata ushawishi mkubwa sana kutoka kwa Wilbraham Slaa na Lipumba ambao walisemekana tokea mwanzo walianza kuonekana na dalili za kutumiliwa na CCM.

Kwa upande wa Wazanzibari walio wengi hawana imani sanaaa na viomgozi wa Upinzani kutoka Tanganyika, hasa wale walioshika nyadhifa  kubwa za  Utawala wa CCM.

Tulikuwa tukijiuliza Kulikoni Lowassa kutoka CCM?

Na sasa tunajiuliza who will be next to move from the opposition party to the Dictatorship party?

Kulikoni Sumaya kutoka CCM? Na lini na yeye atarudi CCM?

Katika makala hii nitapenda kuchambua sababu 3 kubwa zilizomuhamisha Lowassa kutoka Chadema au ukawa na kurudi  kwa mama na baba yake CCM alikozaliwa CCM nazo ni:-

  1.  Personal Issue, (kuogopa kuporwa mali zake alizochuma akiwa madarakani, kumnusuru mkwe wake anaesota jela kama akina Mbowe
  2. Kuto kuaminiwa na CMD Conservartive.
  3. Lowasa si chaguo la Uraisi ktk UKAWA/ Chadema.

 

1.Personal Issue:

Kama ni livosema Lowassa nikiongozi mkimya ambae tokea alipotoka upinzani alikuwa kimya tuu na amekaa kimya kwa kuogopa kuikosoa CCM na kuhatarisha mali zake alizoi zichuma akiwa kiongozi wa CCM miaka mingi. Tumeweza kumuona katika campeni za Uchaguzi wa 2015 Lowasa alikuwa najuwa siri nyingi sana za CCM na uharibifu wa mali za umma ambazo hutumiwa kwa shuhuli za kichama. Lowassa alijuwa kwamba  ESROW ni sakata lakulitumia kuikosoa CCM lakini alikaa kimya. Kimya kile ni kimya chakuzuia Maovu ya CCM ili wasije kumdhuru yeye na familia yake.

Hivi sasa mkwe wa Lowasa anasota ndani / amebandikizwa kesi nyingi sana na CCM kama ilivo kawaida yao kuwabandikiza kesi Wapinzani. Jambo hili limemfanya mtoto wa Lowassa kupata shida yakukosa mume na kuachwa  na watoto peke yake. Hii nayo ni sababu kubwa ya Lowassa kurudi CCM. Na analysis yangu inanambia kwamba CCm wamemuahidi kumtoa mkwe wake na kumfutia kesi zote zakubandikizwa mapema mwezi huu. Kama Wananchi wa Zanzibar na Tanganyika hamuamini mutakuja kunambia.  Lowassa aliwahi kuhusishwa na uchau wa mali ya umma ya ESROW,ili kuinusuru mali na nafamilia yake isiguswe ameona aingie CCM kabla ngoma haija pamba moto. Na kwakumfurahisha Mfalme Pombe si ajabu kuona anatoa data za uongo kuhusiana na CDM. Lowassa ana mafao makubwa ya kutoka kwenye mfumo wa CCM, ili apate alipwe mafao yake yasije kukatwa na utawala huu wa CCM ambao sasa umeanza kuwadhulumu wafanyakazi na Pension zao. Kwa Lowassa mali ni bora zaidi kuliko  Uzalendo na kuiona jamii ina utawala bora unaoheshimu Democrasia, Civic Rights na kuwatumikia wananchi hao kwakuheshimu Katiba za Nchi.

Kwa upande wa point hii ya kwanza kuondoka kwa Lowassa CDM hakukuleta madhara bali CDM itaweza kufanya na kupanga shuhuli zake kama inavotakiwa bila yakuogopa nani anaweza kutambua mikakati yao. Jee Chadema inaweza kupiga hatua kwakuondoka kwa Lowassa? Chadema ina uwezo mkubwa wakuchukuwa nchi kama wataweza kuwatumia Wananchi ambao hawafurahisahwi na utawala wa Mabavu uliopo madarakani kwa miaka nenda miaka rudi. Tatizo liko hapa jee Chadema woote ni Wazalendo ambao wanasimamia wanaloliamini? Au ni kama akina Lowassa, Mtatiro, Lipumba na wengineo?

 

2.Kuto kuaminiwa na CMD Conservartive.

Lowassa ameingia Chadema miaka 4 sasa, lakini kuingia kwake kulikuwa ghafla na kutoka kwake ni ghafla na kusahauliwa kwake katika Jukwaa la Siasa kutakuwa hivo hivo. Lowasa alipoingia Chadema kulikuwa na wafuasi na viongozi wengi hawakutaka Lowassa apewe nafasi ya juu just like that. But he got it however, he did not have all access information about Chadema Privacy. Lowassa alikuwa anafuatiliwa nyendo zake na hata kampeni zake za 2015 ndani ya Chadema, Lowassa alishindwa ku-deliver as Chadema as they ware expected to. Hata hivo aliweza kumshinda Magufuli katika Uchaguzi wa 2015, na kama Tume ya Uchaguzi Tanganyika ingekuwa Huru na ya Haki Magufuli asinge kuwa na Majority kwenye parliment. Lakini ndio hivo tena CCM ushindi ni lazima hata kwa kushinda kwa kutia GOLI la MKONO.

Kutoka kwenye zile campeni Chadema ilianza kuona kwamba Lowassa hawafai na walimtilia wasi wasi sana. Tumeweza kuona matokeo mengi ya ukiukwaju wa Democrasia ya vyama vingi yanatendeka, na hata kupigwa kwa risasi Mh. Tundu Lissu. Tulitegemea Lowassa asimame kulaani sana tokeo lile kama Mtanzania lakini sijuwi kama alinyanyua mdomo wake. Matokeo mengine yanyanyaswaji wa Viongozi wa Chadema na uharibufu wa mali zao, Lowassa kimya. Na kwakuwatukana Chadema matusi ya nguoni zaidi Lowassa alikuwa akimsifia raisi Magufuli na utendaji wake na kusahau his other side of Iron Leadership. Hili nalo lilishawatia Chadema Wac wac nakuanza kumyima access za siri za Chama.

Kwa point hii Chadema hawakuumia  kuondoka kwa Lowassa  kwani Siri za Chama na Mikakati yao hawakumpa Lowassa tokea siku alioingia kwenye Chama. Jengine, anapingana na mawazo ya Chadema kuiletea Tanganyika Ushindi na utawala bora wa sheria na katiba  na kuunda Muungano wa Serikali 3.  Lowassa anaamini mfumo wa Serikali 2 kuelekea moja na Zanzibar kumezwa ndio ajenda za Viongozi wengi wa Tanganyika ambao hawajuwi Consequence ya Ukoloni Mambo leo. Lowassa aliwahi kumuuliza maalim Sefu , ni kwanini anataka kuvunja Muungano? Lowassa anaamini Muungano wa Kuchanganya Mchanga wa Tanganyika na Zanzibar kwasababu anaefaidika ni Tanganyika na sio Mzanzibari. Lowasa hajali hata maslahi ya Indiginal Masai people ambao hadi sasa wanaishi kwa kunyanyaswa nyanyaswa. Hivo Lowasa amewapatia Wapinzani Kupumua. Labda kwa mabwege wasio juwa wataona kwamba Chadema imeumia.

 

3. 2020 Lowasa si chaguo la Uraisi ktk UKAWA/ Chadema.

Uchaguzi wa 2020 ni uchaguzi ambao kama Watanganyika watakuwa kweli wanataka Utawala Bora na wa Kidemocrasia basi  wanaweza kuiondoa CCM. Kwahivo ukitaka kuiondoa CCM ni lazima uweke kiongozi mwenye Kujuwa Sheria za Nchi na kuheshimu Sheria hizo pamoja na Katiba. Hadi sasa kiongozi anaetetea haki za Nchi na Utawala wa Haki ni Mh. Tundu Lissu na kidogo Zitto Kabwe ana mvuto. Na sio Lowassa. Sasa Lowassa kubakia Chadema anaweza kukosa mtoto na maji ya moto alo na waswahili wa Kizanzibari. Na kukosa mtoto nikuwa kama kivuli ndani ya upinzani na kukosa haki zake na heshima za mali zake kule CCM. Hivo ameamuwa kujitowa mapema ili aweze kujilinda yeye binafsi. Na si vyengine. Lowassa hana point zaku argue kuhusiana na utendaji wa CCM kwani atakuwa anajisuta yeye mwewnyewe kwavile alikuwemo kwenye mfumo nakuyaona machafu yoote yaliofanywa na CCM. Mh Tundu Lissu na Zotto kabwe wanaweza kuichambua CCM ndani  na nje kwa faida ya wananchi. Hata katika campeni  za 2015 Lowasa hakuweza kufanya mabishano mazuri ktk campeni zake za Uraisi. Sijuwi alikuwa akiogopa au akiona anajisita yeye kwa yeye?

Hivo kwa point hii vile vile Chadema naamini wamepumua sana na kufurahia kuondokwa kwa JIVULI la MVUMO lisilo na Faida. Kuhusu Kuondoka na Watu, Lowassa ataondoka na Watu ambao hawajijui wala hawajitambui kama hao akina Dimond na wanamuziki au Wana habari wengine waliokuwa hawajuwi umuhimu wakuijuwa katiba ya nchi yao nahaki zao. Kwa Upande wa Wazanzibari, Lowasa na akina Sumaiya cc tunawaona ni wafuata nyuki. Inawezakuwa malim Sefu personal anamuheshimu na kumsamehe Sumaiya lakini Wazanzibari katu hatuwezi kuwasamehe Viongozi wa Tanganyika CCM.

Share: