HabariHabari-PichaMatangazo

Maombi ya Msaada

MSAADA WA KUMALIZIA JENGO LA MADRASAH MKWAJUNI ZANZIBAR NI SHILINGI 4M ZINAHITAJIKA.

Allaah Anasema:
“Chukuwa Sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao)”. At Tawba – 103
Kwa niaba ya Madrasah ya Mkwajuni nawaomba Waislamu wote popote walipo kutoa sadaka zao kumalizia jengo hili ili wanafunzi wapate sehemu ilio nzuri kwa kusoma dini yao.
Mazingira ya kusomea yakiwa mazuri basi na mafanikio pia huwa mazuri.
Sina haja ya kueleza mengi kuhusu faida inayopatikana katika kutoa sadaka kwenye majengo ya elimu hasa ya Ibada.
Moja kati ya hizo ni kama hadithi ifuatayo:
Amesema Mtume Swalla Llahu Alayhi Wasallam.[Atakapo kufa mwanaadamu hukatika matendo yake ILA katika matatu;sadaka yenye kuendelea au elimu yenye kunufaisha au mtoto mwema mwenye kumuombea mzazi wake] Muslim.
Miongoni mwa sadaka yenye kuendelea ni kujenga au kushiriki katika kujenga kisima, msikiti au kupanda mti ambao viumbe vitanufaika nao n.k.
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah anasema: ‘Ewe mwanadamu, toa na sisi tutakupa”
Yeyote atakaenafasika kutaka kutarazzak kwa jambo hili unaweza kutoa mchango wako kwa kupitia paypal ya mzalendo.net

Na Kwa waliopo Nyumbani wanaweza kuchangia kupitia TIGO Pesa nambari 0716536666

Kwa waliopo UK na hawana account na Paypal mnaweza kuwasiliana na nambari 07588550153

Shukran

e60efd0d5106f2df0c57afee30e9adcd

709d5c033af6a2737695914329f1c5fb

83afa6a722fd268c6a10566e4a259463

7b9be91e9b77084b6f20737827d0f21d

6e01f07944b2fb3b6199763cc7f2f008

3e32b329ea227ca221dabf508147be68

Tagsslider
Share: