HabariZenjiLikiz

Mapinduzi II na ufisadi.

FB_IMG_1449365670668
GPS data zinasoma kwamba kuna meli inayoitwa POSCO PLANTEC 13SV01, IMO No. 9708485, Call Sign 51M254, ambayo katika database ya AIS (Automatic Identification System) inaonekana kama MAPINDUZI II, iko Zanzibar kama inavyoonekana katika picha.

Hii ina maana kwamba katika database za Maritime, bado inaendelea kujitokeza kwa jina lake la asili. Sisi walipa kodi wa Zanzibar tuna haki ya kuhoji kama kweli meli ni mpya au reconditioned.

Tukumbuke kuwa IMO number haiwezi kubadilika, hata meli itakapobadilishwa jina, mmiliki au kampuni kwa sababu ni nambari inayotumika kwa sababu za kiusalama na kuondosha udanganyifu katika soko la Marine. IMO ya Mapinduzi II ambayo imechorwa ubavuni, nyuma upande wa kulia ni 9708485. Namba ile ile kama ilivyokuwa katika registration ya jina la POSCO PLANTEC 36SV01.

Tunataka kuamini kwamba ni mpya, lakini hali ya meli yenyewe na information zinazojitokeza zinaendelea kutusuta kwamba ni kinyume chake.

Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa jicho pana hasa ikizingatiwa imetumia pesa nyingi sana (dola za Marekani milioni 30.8) na kama ikigundulika kumefanyika ufisadi, basi wahusika wachukuliwe hatua haraka kwa style ya Rais Magufuli.

Wakaguzi wa nje wa Serikali wapo (nitatoka likizoni ikibidi) na wana taaluma ya kutosha katika masuala ya procurement. Watumike hawa kufuatilia hili.

#MagufulificationIsRequired #tusimezeeubadhirifu

Share: