Habari

MAPINDUZI: Katika Siasa ni Kitu kisicho epukika.

BY Chatumpevu

Mapinduzi ktk siasa ni kitu kisichoepukika. Kilicho wazi ktk siasa za CUF hivi sasa ni kuwa mapinduzi ya nguvu yamefanyika kwenye safu ya uongozi ya CUF baada ya msaliliti Lipumbavu , kwa kubebwa na tasisi za serikali ( polisi, RITA, ofic ya msajili, mahkama na mkono wa serikali- executive arm ) wameweza kumuondoa maalim seif ktk nafasi yake ya ukatibu mkuu wa chama. Kwa tukio hili, pengine, CUF ya msaliti lipumbavu, serikali za CCM ( SMZ/SMT) wameona ni ushindi mkubwa. Kwa mtazamo wa haraka unaweza ukaamini hivyo kwa kuwa ule uimara, umahiri na popular support ya CUF sasa itakuwa iemeathirika. Safu ya uongozi wa CUF , sasa imeshakuwa na uongozi mpya, uongozi ambao, umewekwa ili kukamilisha matakwa ya serikali za SMZ/ SMT ya kuua nguvu za CUF Zanzibar na sio bara kutokana na trend ya ushindi wa chama hiki ktk chaguzi zote toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Mkono wa serikali za CCM ni mrefu hapa na umekuwa na role kubwa ya kuigawa CUF na hatimae kuidhoofisha kabisa. Suala muhimu ni jee, hali hii iliyojitokeza itabadilisha vipi political landscape ya Zanzibar? Jee, wapenzi wa CUF iliyokuwa ya maalim seif watabaki kuwa ni wananchama watiifu kwake au watauunga mkono uongozi mpya wa CUF ya wasaliti? Nini athari ya mabadiliko haya ya uongozi kwa mustakabali wa siasa za znz? Masuali haya hayana majibu kama kero za muungano.
Kwa upande mmoja, pengine, serikali za CCM zinaweza kuona kuwa sasa wameshafanikiwa kuidhoofisha CUF na kuweka CUF yenye baraka zote za kitaasisi na kisheria ( unless uamuzi wa makhakama utakaofanywa ksho tarehe 18/3 ktk kesi ya msingi ya uhalali wa uenyekiti wa lipumbavu alipojiuzulu na akaamua kurudi tena ktk nafasi ile ile utaamua vyenginevyo).
Wachambuzi wa siasa, wanaweza wakaja na analysis nzuri itakayoonesha athari ya vuguvugu hili la mabadiliko ndani CUF.

Bado, kwa mawazo yangu, nafikiri CCM/ SMZ/SMT hawajakuwa na uhakikia wa 100% kuwa dhamira yao imetimia kwa sababu hawajajua ni upi utakuwa msimamo wa wananchi walio wengi na ambao ndio wanaomuunga mkono Maalim Seif. Kundi hili ndilo linaloonesha popular support kwa maalim na ni kundi muhimu ambalo lita – shape mwelekeo mpya wa siasa za znz. Kama serikali za SMZ/ SMT litashindwa kulidhibiti kundi hili linalomuunga mkono maalim seif itakuwa ni sawa na kujipaka mavi kwa serikali kwa kujidanyanganya kuwa wamemaliza tatizo. Kumbe, wafuasi ndio mtaji muhimu wa kiasiasa (political capital) popote pale na hususan ktk siasa za kwetu znz.

Mpka sasa SMZ/SMT/ CCM na CUF wasaliti hawajajua CUF ya maalim itachukua hatua gani na upi utakuwa mwelekeo mpya? Ni changamoto ngumu ambayo itawaumisha vichwa CCM na CUF mamluki kwa siku nyingi. Hii ni transition muhimu inayotoa somo la kujifunza. Mambo mengine hayawekwi hadharani lakn kama CUF ya maalim itaamua kushirikiana na chama kingine (temporary solution) na huku , baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 wakaja na suluhisha la kudumu la kusimama kama chama kipya, naamini itakuwa ni pigo kubwa kwa CCM/ SMT/SMZ ktk kisanduku cha msemakweli kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 and beyond kwa kuwa wafuasi ambao ni loyal kwa maalim watakipigia kura chama hiki ambacho kimeungana na CUF ya maalim. Wafuasi hawa bado wana Imani kwa maalim na wanawaona CUF mamluki ni agents na puppets( vibaraka) wa kuendeleza ukoloni wa kuitawala znz kupitia dhana ya wagawe na uwatawale ( devide and Rule).
Sintofahamu hii ambayo imekidhoofisha chama cha CUF nimeipachika jina la ‘Mutungi Syndrome ’ itaifanya siasa za znz kuwa ni za uadui zaidi kwetu sisi wazanzibari kwa kuongeza kundi jengine pinzani na hasimu, kundi ambalo litakuwa likibebwa na taasisi za dola kima kinavyobebwa chama cha CCM.

Jambo miuhimu kwa sasa, viongozi wa CUF ya maalim waoneshe ubunifu zaidi wa kifikra ( creativity) na wasi panick kutokana na dhorba hii ya IDAI ( kama ile ya Msumbiji iliypotokea wiki jana), washikamane zaidi na waione the big picture ya siasa za Znz.
Hatua zozote watakazochukua zibuniwe kwa uangalifu mkubwa na kwa kweli , kwa hali iliyo, bado CUF ya maalim inaungwa mkono na wananchi wengi zaidi. Nini kifanyike kwa sasa?. Mambo matatu yanaweza kuzingatiwa:
1. Kutafuta platform ( hatua ya muda) ya kuuungana nayo ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi wa mwaka 2020. Hatua hii iwe ni ya muda ili baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 wafikirie kusajili chama na kuweza kurejesha identity ya kisiasa kwa wazanzibari
2. Kufanya mikutano ya kuwarejesha matumaini wananchama loyal kwa pande la CUF la maalim ili waendelee kuunga mkono juhudi za kurejesha uzalendo wa znz.
3. Kuanza kufikiria hatua za kimkakati za kuchukua ili ule uungwaji mkono wa pande la maalim uendelee kuwepo sambamba na kufikiria candidate mpya atakayesimama kwa nafasi ya urais wa zanzibari wa mwaka 2020 badala ya maalim seif ktk hiyo platform watakayoamua kuungana nayo.

Share: