BarazaniHabari

Marufuku ya vimini kutekelezwa hivi karibuni

ZANZIBAR: Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema mpango wa kuweka sheria ya kupiga marufuku vimini (viguo vya nusu uchi) kwa umakini ili kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa ili uvaaji wa nguo uwe stahiki.

Wiraza Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Wizara ya Katiba imeahidi kukaa pamoja kuhakikisha sheria inayokataza watu kuvaa vimini inatekelezwa kwa kuwa tayari sheria hiyo ipo lakini utekelezaji wake ndio bado haujafanyika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Fatma Abduhabib Fereji wakati akijibu suali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma alietaka kujua serikali ina mpango gani wa kurekebisha uvaaji wa nguo zisizostahiki na kupelea vishawishi vinavyoweza kuongeza ongezeko la mambukizi ya VVU hapa Zanzibar.

Waziri Fatma alisema wanaendelea kufanya mapitio sera yao ya kitaifa ili iendane na mabadiliko ya mkakati wa kitaifa ili iwe dira ya mapambano itakayofuatwa na wadau wote katika mapambano hayo kwani rasimu iko tayari na karibu itapelekwa serikalini kupatiwa idhini.

Akitoa majibu ya nyongeza juu ya suala hilo, Waziri wa Afya Juma Duni Haji alisema alisema bado utekelezaji wa sheria hiyo unaweza ukawa ni mgumu kutokana tendo la ngono linafanyika kwa usiri mkubwa na ni vigumu kuweza kubainika mara moja.

Alisema kiwango cha mambukizi hivi sasa kimeonekan kuongezeka zaidi kwa watu wanaotumia dawa za kulevya ambao hutumia shindano kujidunga ambapo maambukizi yao yapo kwa asilimia 16, huku wanaojiuza miili yao ni kwa asilimia 10.2 na wale wanafanya vitendo vya kujamiana kwa kuingiliana wanaume kwa wanaume ni asilimia 12.3.

Aidha, Waziri huyo alisema tayari serikali imeshafanya mapitio mkakati wa kitaifa wa kupambana na makundi maalum yenye viwango vikubwa vya maambukizi zaidi ya asilimia 10 ikilinganishwa katika jamii kwa ujumla asilimia 0.6.

Duni alisema suala la mavazi aina ya vimini sio sababu kuu ya msingi inayochangia kuongezeka kwa maradhi ya ukimwi ila kumekuwa na tatizo kubwa la watu kushindwa kupambana na nafsi zao kuacha kufanya ngono.

Alisema baadhi ya mataifa duniani, wavazi ya vimini ni sehemu ya utamaduni wao, lakini bado wamekuwa na kiwango kidogo cha maradhi hayo kwa vile watu wao wamekuwa wakipambana binafsi na ugonjwa huo.

“Sababu kubwa na ngumu ni vita vya nafsi, ambavyo viko katika uhuru wa binadamu kwa kutokatana kufanya vitendo vya ngono na sio vimini peke yake hivi hata wakivaa kama hawafanyi ngono hatapata ukimwi ila tatizo tunashindwa kupambana na nafsi hili ni jambo zito sana” Alisema Waziri huyo akimaanisha huo ni uhuru wa mtu binafsi.

Waziri Duni, amesema kuwa tatizo la kuongezeka kwa maradhi ya ukimwi Zanzibar halitoakani na uvaaji wa vimini tu kwa Waanawake bali jamii inashindwa kupambana na vita vya nafsi jambo ambalo linahitaji elimu zaidi kwa umma.

Aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba njia kuu ya kuweza kupambana na maradhi hayo ni namna ya serikali itavyoweza kujipanga kuendesha kampeni kubwa itayosaidia kukabiliana na ugonjwa huo.

Tagsslider
Share: