Habari

Shekhe Ramadhani: Fatwa yako ilipangwa na CCM/CUF:

Ndugu zangu wasomaji wa mtandao hii, leo mchana katika kupita pita yangu niliona CLIP yenye ujumbe ”  Mashekhe wa DAR Wamuonya Zitto Kabwe kuhusisha Siasa na Dini. Na hio nafikiri ni FATWA ya Mashekhe hao. Bila yakurudia nini alisema Mh. Zitto kabwe kuwataka Mashekhe watowe ushauri wa jambo hilo. Nakuja kwa huyu Shekhe anaeitwa Shekhe  Ramadhani na mkuu wa Maimamu DAR.

Ukweli tulioupata kutoka ndani  ya inteligensia nikwamba,ccm CUF ya Lipumba- furaha yao wanataka Chama cha ACT-Wazalendo kifutwe. Ili wale maaduwi zao wasiwe na pakushika. Hivo basi kwavile wana pesa nyingi za Ruzuku, ambazo ni kama billion moja na upuuzi, wamewalipa baadhi ya Mashekhe njaa  ili waje watowe FATWA na kumlaani Zitto Kabwe na Maalim Sefu Sharifu. Jamani Mtu amewaachia Chama bado muna msakama sakama . Lipumba amesikika akisema Maalim Sefu amekwenda kutia Kirusi ACT-Wazalendo, pia Lipumba akliwahi kusema wiki iliopita kwamba chama cha ACT-Wazalendo kitapotea karibuni hivo aliwaomba Wazanzibari wasimfuate maalim Sefu.

Pili waliona wakifanya hivo Msajili MUTUNGI atakuwa na sababu yakukifuta chama hichi cha ACT-Wazalendo na wao ccmCUF lipumba watapata wanachama wao waliotoka CUF iliouliwa na CCM na kuingia ccmCUF ya Lipumba. Kwa taarifa za Wazanzibari, hakuna asie wajuwa kama watu hawa wame base sana kwenye dini, na hutumia neno Allah akbar allmost kila sehemu, na wala hakuna uharamu wowote ule. Hivo tunaamini kwamba, ccmCUF-Lipumba lengo lao sio kujenga chama cha CUF kama anavojidai ila ana lengo lakutaka Roho na Damu za Wazanzibari sasa. Kwasababu hapa tatizo sio ACT-Wazalendo; Ni mwaka wa 4 huu tokea ACT Wazalendo isajiliwe , hatujasikia  chama hichi kuandamwa na CCM au CUF Lipumba. Lakini tokea Wazanzibari walipoingia katika Chama hichi, tunawaona Wabaya wa Zanzibar na Wazanzibari jinsi wanavo hahah kama Mbwa Mwitu.

Mimi binafsi kama Mzanzibari sina Imani na Mashekhe wengi wa Kitanganyika  hasa hawa mashekhe wanaojipendekeza na Magufuli au Serikali ya CCM- Mashekhe wakuaminika haswa wenye Elimu ya dini ni Shekhe ILUNGA, Allah amrehemu na amuweke katika Janna na Shekhe PONDA, Allah ampe umri mrefu na afya njema Amiin.

Mashekhe  kama huyu Shekhe Ramadhani  ni aina ya  wale akina Mashekhe walioshindwa kutetea Haki za WaISLAMU WA TANGANYIKA – za kuwapatia Waislamu Mahakama ya Kadhi. Ambayo wamekuwa wakiililia kwa miaka mingi sana. Na mashekhe hawa ndio katika wale walioingia katika Bunge la Rasimu ya Katiba 2014 na Kumlilia Nyerere. Kwamadai kwamba Nyerere Ati alitukanwa. Hawa ni mashekhe wanafik sana kulia kwa ajili ya Nyerere. Nakuacha issue zao muhimu ambazo zinakandamizwa na Serikali hii ya Mfumo Kristo kwa miaka 57 tokea Tanganyika wapate Uhuru.

Nikija kwenye Mada: Shekhe huyu anaeitwa Shekhe mkuu alisema katika taarifa yake kwamba aliwasikia watu wakisema TAQBIR ile tunayosema wakati tukiona mwezi au Tukiwa tunataka kusali sala za EID.. Mimi kwa ufahamu wangu Taqbir nilioisikia ni ile Unayosema Allah Aqbar tu.

Sasa katika Fatwa yake amemlaumu Zitto kabwe nakulaumu Chama cha ACT kwamba kinaingiza Dini katika Siasa.

Hivo Shekhe huyu tukimuuliza sijuwi anaweza kuona na kupambanua Chama kinachotumia fedha za Walipa kodi na kupromote Udini basi ni CCM. Na walifanya hivo hata katika Bunge la Katiba. 2014. Hatukumsikia Mutungi kusema neno lolote au kuja mashekhe kulalamika. Bunge lile lilokuwa linataka kujadili Rasimu ya Warioba lilisomewa MISA ndani ya Bunge siku 3 kabla Vikao vya Bunge havijaanza. Mimi naweza kusema ulikuwa kama Ushirikina hivi. Wakutaka Kuwatiribua Wapinzani na Kupindua matokeo ya Rasimu ya Warioba ili waweke Rasimu ya Christian Catholics Movement CCM.

Mashekhe hawa baadhi yao walikuwa mule ndani na ndio waliojitia vilio wakati watu waliokuwa wanapinga Muungano wa kuchanganya Mchanga na Mkataba wa Muungano aliouunda Nyerere kuhojiwa.

Sasa cc Wazanzibari tumekuwa kama Mayatima, hatuna pakukimbilia, kwasababu Mashekhe wetu wametiwa ndani mwaka huu wa 7 sasa. Tunataka hawa mashekhe wengine walioko Nje watwambie . Jee Takbira ile moja iliosomwa ilikuwa inamaanisha Udini au Ilikuwa ni kama Kujipa matumaini kwa Wanachama walionyanganywa haki zao October 2015. Nakunyanganywa Chama chao 2019?

Jamani tuangalie binaadamu kwa roho za kiislamu au hata kibinaadamu na Sio kishetani na Kimatumbo yetu. Wazanzibari ni watu ambao wanastahili kusifiwa pamoja na Viongozi wao kwa Uungwana na Utiifu wa kudumisha Amani walioufanya tokea 1995 hadi 2019.. Muda wote huo walikuwa hawana mtu wakuwasemea wala bega lakulilia. Na  pale walipopata bega la kulilia katika chama cha ACT wanakumbuka jina la Muumba wao nakusema Allah Aqbar yaani Mungu Mkubwa. Pana ubaya gani hapo jamani?

Mas

Share: