HabariMaoni

Matokeo kwa mujibu w CUF : Zingatia sharia ya ZEC

Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni. Mengi zaidi, sikiliza matangazo yetu ya leo mchana.

Hisabu za HARAKA HARAKA

Waliojiandikisha wote kwenye ZEC ni 503848 (Registered voters)
Kati ya Hao kuna watu waliokufa (Deceased) (unknown number)
Kuna watu wasio na Sifa ya kuchagua Rais wa Zanzibar (not declared by ZEC)
Na kuna watu waliopiga Kura (TURNOUT)
Na kuna Kura zilizoharibika (Invalid Votes)
Na kuna Kura zilizokuwa sahihi (Valid Votes)

Tukichukuwa Kura zote za Maalim Seif tukijumlisha na za Dr. Shein ukiachana na maelezo ya hapo juu tunapata jumla ya kura 378,363 tuchukue hao wote 503840 ni wapiga kura wenye haki ya kupiga Zanzibar urais tunapata 75% turnout roughly.

Inamaanisha watu kiasi cha 125485 hawakupiga kura au hawana sifa za kupiga kura urais Zanzibar au ni invalid votes au hata wamepigia vyama vyengine..

kwa maana hiyo Dr.Shein atakuwa amepata 47.1% kati ya 52.9 % CUF Roughly .. not even closer
Tume ya uchaguzi kupitia kwa Mkurugenzi wa NEC akiongea na ITV jana tar 25 alisema Matokeo yote ya Unguja na Pemba na mikoa yote ya Bara wanayo,cha kushangaza ZEC wamesema wana matokeo ya majimbo 2 tu ukiacha yaliyoainishwa leo mengine ya Chwaka kuwa CCM wameshinda pia.

Kwa mujibu wa sharia ya tume ni kuwa Hadi mgombea atakapotangazwa na mawakala wa tume ndio atakuwa mgombea halali na sio kwa mujibu wa form zinazosambaa..

Lazima mgombea atangazwe

pia zingatio jengine ni kuwa : Form za mawakala wa CUF sio form za TUME hadi tupate form zilizokuwa verified na tume ndio tuanze kusherehekea.

Maalim amesema wazi ” kwa mujibu wa form za mawakala wao ” na sio form za ZEC wala NEC ijapokuwa zinachapishwa tu na NEC/ZEC ..

Mungu Ibariki Zanzibar..

(source yangu mwenyewe + CUF data)

Share: