Habari

Sultan Jemshid ni mzawa wa Zanzibar

MFALME ALOPINDULIWA SAYYID JAMSHID
Sultan Jamshid
Nyerere alikua na lake moyoni (agenda ya siri)alishiriki kumtorosha huyu ili apate kui Koloni Zanzibar kwa Kisingizio cha Ubaguzi wa Kiarabu na Sultani.

Sayyid Jamshid hakuja Zanzibar kama mgeni kutoka Arabuni, Sayyid Jamshid Kazaliwa Zanzibar na kasoma Zanzibar mpaka kamaliza na kaondoka Zanzibar baada ya kupinduliwa na Kapitia Bandari ya Dar es Salaama kuelekea Uengereza (Portsmouth)alikokwenda kuomba Ukimbizi , kwahio Jamshid ni Mzanzibar kama wengine walozaliwa Zanzibar na kuwa na haki ya Uzaliwa.

Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliupindua utawala wa kiarabu tu ,lakini sio kupindua haki ya Wazaliwa wenye asili za Kiarabu, kihindi, kingazija , generation yote ya vizazi hivyo sasa ni Wazaliwa wa Zanzibar na wana haki kama wale wazaliwa wa Tanganyika akina Nyerere, na Ali Hassan Mwinyi na Mpaka Kikwete mwenyewe.

Sasa ukisema watu hawa wenye asili za kiarabu ,kihindi na kingazija Unawabagua haliyakua ni Wazaliwa wa Zanzibar na huwataki unataka Wahame Kikwete na ccm yako, jee tukikuliza utawapeleka wapi?

Wewe Mwenyewe Kikwete uko tayari kuhamishwa Bwagamoyo Tanganyika?

Wznz tumechoka na ubaguzi wa ccm wakutugawa kwa misingi ya hii ya Uarabu(Usultan ) Uhindi ,Ungazija,Upemba na kubwa zaidi sasa ni karata ya Undini ambayo ni kuomba huruma kwa mataifa ya Magharibi kuja Zanzibar ku deal na Waislamu wa Zanzibar ? maskini ccm Smz kupoteza muelekeo hata wa Dini yao kwa TONGE, Waislamu wa Zanzibar si 0% ni %99 sasa unapo tumia U-dini kwa kukiimarisha chama Basi utafeli tu .

Makabila yote hayo nilioyataja hapo juu hakuna alokaribishwa Zanzibar wote ni Wazaliwa wa Zanzibar kulikoni hata Ali Hassan mwinyi na Wenzake walokuja Zanzibar kwa kukaribishwa sio Uzawa, katu huwezi kumlinganisha U-Zanzibar wa Ismail Jusssa, Eddy Riam , Maalim Seif ,Maalim Haroun, Salim Dimani na wengine kua ni sawa na Ali Hassan Mwinyi ambaye sio Mzaliwa wa Zanzibar .

Mwinyi hana sifa ya Uzawa wa Zanzibar lakini hao wote wana sifa ya uzaliwa wa Zanzibar na si watu walozaliwa nje ya Zanzibar wamezaliwa Zanzibar na kusoma na kumaliza Zanzibar hata huyo munaye mwita Sultan Jamshid , kwa hio ccm wacheni karata ya kubagua jamii ya Wananchi wa Zanzibar kwa misingi ya Ubaguzi wa rangi .

Visiwa vyetu viwili vya Zanzibar vina mchanganyiko wa makabila na wa rangi , kama badhi ya visiwa vingi ulimwenguni vina sifa hio.
Sasa ccm Munapo tumia siasa kwa kubagua jamii hili hatutolivumilia hususan hapa kwetu Zanzibar, ccm Smz tutapambana na nyiyi kwa jambo hili mpaka kiama na ni haki yetu.

Unapoleta kuwagawa Wazawa wa Zanzibar kwa misingi ya rangi zao na asili zao, hii itawa-cost sana ccm na mwicho wa hayo ni kufilisika kisiasa na chama chenu kukosa Dira na muelekeo na kuachiwa wenyewe munaojita WAHADIMU mukiongoze chama chenu cha Ubaguzi?.

Hivi sasa Takriban Wananchi wa Zanzibar wamechuhudia mengi yalokuwemo kwenye nyoyo zenu , juu yakua Bunge la katiba halijulikani kua litaendelea au vipi ? lakini tunamshukuru Allah kuona yale muliokua nayo katika Nyoyo zenu.

M/mungu ibariki Zanzibar na watu wake wote.

Share: