Habari

Mh,Bimani:awaasa wananchi wa kichaka kuutumia vyema mwzi mtukufu wa Ramadhan

Wananchi wa kijiji cha kichaka jimbo la kiwani mkoa wa kusini Pemba wametakiwa kuzidisha umoja na mshikamano wao walionao hususani katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu ramadhan.

Kauli hio imetolewa leo mwezi 19 Ramadhan na mkurugenzi wa haki za binadamu habari uenezi na mawasiliano ya umma Mh,Salim Bimani wakati alipomuwakilisha makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad aliposhiriki katika ftari maalumu ilioandaliwa na wananchi wa kijiji hicho.

Pia Bwana Bimani amewaasa waislamu hao kuutumia vyema mwezi huu mtukufu kwa ajili ya kufanya ibada pamoja na kuomba msamaha kwa mola wao juu ya makosa mbali mbali wanayoyajua na wasioyajua.

Aidha amesema kuwa amefurahishwa sana na ukarimu wa watu wa kichaka dhidi yake kwani hii si mara ya kwanza kuhudhuria katika ghafla ya ftari kama hio na wamekuwa wakumpokea vizuri pamoja na kumthamini.
‘’Naomba nichukue fursa hii adhimu kutoa shukrani zangu za dhati kwenu nyote kwa kuonesha kuwa munanijali kwa kiasi kikubwa’’alisma Bimani.

Pia aliwasisitiza wananchi hao kudumisha umoja wa wazanzibar hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi yetu ya Zanzibar imekabiliwa marekebisho makubwa ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Sambamba na hayo alitumia nafasi hii kuwataka wajumbe wa mabaraza ya katiba wilaya ambayo yataingia rasmi katika vikao vya kujadili katiba mpya mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa ramadhan kuwa wayatumie vyema mabaraza hayo kwa kuijadili ipasavo rasimu ya mapendekezo ya katiba mpya kwa kina ili kuhakikisha michango yote itakayotolewa iwe ni yenye kuisimamia na kuyadai mamlaka kamili ya Zanzibar.

Amefahamisha kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba wilaya wanamajukumu mazito kwa kuwakilisha maoni ya wananchi waliowachagua katika mustakbali ya kutaka heshma na hadhi ya nchi yao.

Ujumbe maalumu wa chama cha wananchi CUF ukiambatana na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif amba pia ni makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar upo kisiwani Pemba kwa ziara maalumu tangu tarehe 26/7/2013 na utarajiwa kumaliza rasmi tarehe 30/7/2013.

Share: