Habari

Mkosa ni nani? Ile dhambi ya Ubaguzi mumeisahau

Kwako Bi Clara Alphonse

Nimesoma makala yako kwenye gazeti lako la Bingwa. Makala yenye kutaka kuombwa radhi kwa hicho ulichotaja kimetokea au kufanywa, ikiwa ni mtu binafsi au chama cha mpira Zanzibar ZFA. Nikiamini ni mwandishi uliyebobea sikutegemea kuona hoja yenye ufinyu wa kufikiri ilokosa weledi wa uandishi, ilokosa kichwa wala miguu.

Binafsi nimesoma zaidi ya mara mbili hoja zako nakushangaa unaposema “Tanzania ni nchi pekee katika michuano ya Chalenji ambayo iliwakilishwa na timu mbili”. Hili kwanza nikosa waombeni radhi CECAFA kwa kosa la kufanya cheating. Sidhani kuwa katika ya CECAFA inaruhusu nchi moja kuwa na timu mbili. Ingekuwa hivyo Kenya na Uganda wangekuwa wa mwazo kwani probability ya kuchukuwa kwao ingekuwa kubwa.

Bi Clara, fahamu kuwa tuko kwenye mpira, unapozungumza timu zungumza timu na sio udugu tena. Ikiwa ushindi wa Zanzibar Heroes uliwauma, isiwe ndio sababu ya kuchokonowa mengine. Hapana shaka yoyote kwenu nyinyi soka ni uadui na ndio sababu munafanya kila hila na njama na kuonyesha waziwazi uadui huu. Tanganyika ilikuwa na chama chake cha mpira wa miguu kikijulikana FAT (Football Association of Tanganyika), kipi kilichowapata hata mukabadili jina na kuwa TFF (Tanzania Football Federation), kama sio uadui? Anzeni kwanza kuomba radhi. Kwa mwenye ufahamu anaelewa nini makusudio yenu.

Kama si uadui ni nini, unaposema “….wachezaji wa Zanzibar Heroes wakichukuliwa hatua kali na ZFA”. Hata adhabu unatamani utowe wewe. Hivi kweli kama ni mwandishi na adhabu ya kuchukuliwa unapendekeza wewe. Inamaanisha kukerwa sana na laiti ungekuwa na uwezo basi dhamira na hukumu ingewashukia wachezaji wetu.

Kumbe Mwenyekiti wa ZFA alikwisha chukuwa hatua stahiki ya kuomba radhi , ingawa hukuridhika wala hukuitaka kwani ilikuwa hatua ya kiungwana. Ulitamani achukuwe ile ile hatua za kiuadui uliyotamani kufanyiwa. Sijuwi kitu gani ulitaka zaidi ya hivyo, hebu wachagulie adhabu mwenyewe unayopenda. Bado hukuridhika.

Wazanzibar imani yetu nikuwa Taganyika iwe ni majirani au ndugu tumekaliana kiuadui adui, hasa nyinyi wenzetu. Tunaushahidi na matokeo kadhaa wa kadhaa yakiasharia haya. Ni nyinyi waandishi munaoshadidia mgawanyo wa kimaoneo kwa Zanzibar, wakati kwenu kuna ubaya zaidi ya huu. Kuna ukabila, maeneo na udini, huyu Mkiristo huyu Muislam. Na bahati mbaya waandishi wetu mumeichukuwa dhambi ya ubaguzi kama vile wahyi huu (astaghfurllah) ulishushwa kwa ajili ya Zanzibar.

Tumeona mchango wenu pale Zanzibar inapotaka kujitutumua kujiunga na vyama vya michezo, zaidi ya kuibinya na kuikanyaga Zanzibar hakuna msaada mwengine. Hivi huwa hamuoni.

Mkosa ni nani na nani wa kuombwa samahani, Mtanganyika au Mtanzania?

Musitutowe kwenye lengo letu. Tupeni nafasi kidogo, yakimaliza mashindano njooni na hoja zenye mashiko. Wapeni nafasi wachezaji wetu musiwabugudhi wala musiwatie khofu mukawapotezea concentration and focus. Wapeni free hayo maneno yenu tuwekeeni.

Tagsslider
Share: