Habari

Mkurugenzi ZSTC Pemba lawamani

December 6, 2017 Manager Mwanzo 0

Imeandikwa na mwandishi wetu, Pemba

Mkurugenzi mtendaji wa jumuiya ya wazalishaji karafuu Zanzibar Abuubakari Mohd Ali alisema jumuiya yao imesikitishwa sana na hatua ya Mkurugenzi muendeshaji wa ZSTC kuzarau ,kuikejeli na kuidhalilisha ripoti ya rasimu ya utafiti iliyotolewa na mshuri muelekezi wa ZACPO juu ya kuwepo wa mapungufu katika sheria ya karafuu ya mwaka 2011 na kusema kuwa ripoti hiyo imejaa udhifu na haina mashiko.

Aliyasema hayo katika kikao maalumu (Press Conference ) na waaandishi wa habari wa vyombo mbalimbali huko katika ofisi yao mjini chake chake juu ya kusikitishwa kwao na hatua hiyo aliyoita ni ya kifedhuli na kusema kuwa kutokana na elimu yake na cheo chake haikumpasa kufanya hivyo.

Alisema kuwa si jambo la busara kwa mkurugenzi huyo kukataa kuhudhuria katika mkutano wa kujadili ripoti hiyo na badala yake kukaa peke yake na kuanza kuidharau na kuidhalilisha ripoti hiyo ya utafiti

Ali alisema huwezi kudharau utafiti kabla ya kufanya utafiti mwengine utakao kuja kijibu tafiti ya awali.
”alipaswa kuja kwenye mkutano na kutoa maoni yake jinsi alivyoona yeye na sio kukaa peke yake na kuwaita waandishi wa habari kuzidi kuizarau na kuidhalilisha ripoti hiyo, kitaalamu mtu msomi kufanya hivyo ni kukosea ” alisema Ali

Aidha alifahamisha, katika sheria ya karafuu ya mwaka 2011 kuna mambo yanawakwaza wakulima wa karafuu ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kuhifadhi karafuu majumbani mwao zaidi ya kilo 160, kutokusafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyengine hali ambayo inawafanya wakulima kuvunjika moyo na kuhisi kama zao hilo limekuwa ni kaa la moto kwao na sio neema tena.

Aliendelea kueleza, lengo la ripoti hiyo ni kukaa na kuishauri serikali kuzifanyia marekebisho sheria hizo zinazomkwaza mkulima ili kumpa uhuru na hamu ya kulima kwa nguvu kubwa.

”Katika msimu huu kumeonekana vitendo mbali mbali vya udhalilishaji kwa wakulima wa karafuu ikiwa ni pamoja na kuvamiwa majumbani na kuchukuliwa karafuu zao kinguvu kwenda kuuzwa” alisema Mkurugenzi wa ZACPA

Alisema , wanashukuru sana ripoti ya utafiti waliyoitoa haina tofauti sana na iliyotolewa na Banki ya Dunia ambayo imeonesha hali ya umasikini ya wananchi wa vijijini ambao ndio wakulima wa zao hilo.

”Kauli inayozungumzwa na serikali kuwa wakulima wa karafuu ni matajiri kutokana na kuwa na mabilioni ya fedha sio kweli nendeni kawangalieni, msimu haujesha wanavyodhalilika na umasikini” alisema Ali

Aliongezea kwa kusema kuwa jambo alilolizungumza mkurugenzi muendeshaji wa ZSTC kuwa mikarafuu haipungui bali inaongezeka sio kweli kwani kutokana na taarifa alizozipata kutoka idara ya misitu ni kuwa mwaka 1997 Zanzibar yote ilikuwa na mikarafuu 5833100 hadi kufikia 2013 Zanzibar ilionekana kuwa na mikarafuu 3727000, ambapo kutoka mwaka 1997 hadi 2013 kwa Pemba mikarafuu imepungua kwa asilimia 31.4 na kwa upanse wa Unguja imepungua kwa asilimia 65.8.

Kwa upande wake Kassim Othman Kombo mkulima wa zao la karafuu Pemba ambae pia ni mjumbe wa jumuiya hiyo kwa eneo la Mtambwe alisema, alisikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Wete kwa kushirikiana na vikosi vya Tax force kuvamia katika kijiji hicho na kuchukua gunia 10 za karafuu za Oganic kutoka kwa mkulima Kassim Othman, Bakar Mataka na Khatib Said na kukiita kitendo hicho ni cha udhalilishaji na kusema kuwa wao wanatambuliwa na ZSTC na Serikali wenyewe kuwa wanauza karafuu zao kwa njia ya Organic.

”Mkuu wa wilaya amevunja sheria kuwavamia wakulima hawa majumbani mwao kisha kusaka mpaka masandukuni, kuinua magodoro ya vitanda hadi kufikia kukuta vibubu vya watoto wanavyofugia pesa,kwa nini wavamiwe wakulima wa organic tuu na wengine waachwe na vipi unaenda kumsachi mtu bila ya kuwa na Search Woranty , hapa amevunja sheria na hatuwezi kuvumilia”alisema mkulima huyo

Pemba Today

Share: