Habari

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi

Serikali ya Mkoa wa *Mjini Magharibi Unguja* ameagiza kufungwa kwa biashara za baa na maduka ya kuuzia vileo, migahawa ya chakula wakati wa mchana katika Mfungo wa Mwezi mtukufu wa *Ramadhani* .

Maduka na Migahawa inatakiwa kufungwa wakati wa mchana isipokuwa ya hoteli za kitalii katika kipindi chote cha mwezi huu wa Ramadhani. Pia kusitisha kumbi zote za starehe ikiwemo kusitisha kupiga muziki katika kipindi hicho cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa huo, *Ayoub Mohamed Mahmoud* amewaagiza Mabaraza ya Manispaa Mkoa, Wakuu wa wilaya na Masheha kuwaandikia barua ya wamiliki wa baa na maduka ya kuuzia vileo kusitisha biashara hiyo.

“Mabaraza ya Manispaa ambayo ndio yanatoa leseni ya biashara katika nyumba za kuuzia ulevi, kutoa barua za kusitisha leseni ya biashara hii katika kipindi hiki cha mfungo huu,”alisema Mkuu huyo wa Mkoa huo

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanaowatembeza watalii katika maeneo ya mkoa huo kuzingatia mavazi ya heshima katika kuelekea kipindi cha mfungo wa Ramadhani na kwamba ni wajibu wao kuwakumbusha watalii hao kuzingatia mavazi ya stara yanayozingatia maadili

@ *TAREEQ*

Share: