Habari

Mnazimmoja wafunga kamera za CCTV kufuatilia madaktari

October 2, 201

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Afya Zanziabr, Hamad Rashid Mohamed, amewataka wananchi visiwani hapa kuwafichua madaktari wasiowajibika ipasavyo katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Hamad aliyasema hayo jana Oktoba 1 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa baraza hilo waliotaka kujua ni kwa namna gani wizara yake inapambana na watalamu hao wa afya wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Hamad alisema anafahamu kuwa wapo baadhi ya madakatari kwenye vituo mbali mbali vya afya visiwani hapa wamekua wakishindwa kutoa huduma bora na inayostahiki kwa wananchi wanaofuata huduma hizo jambo ambalo halileti taswira nzuri.

Alisema katika kupambana na hali hiyo, tayari wameamua kutumia mfumo maalumu wa CCTV katika hospitali kuu ya Mnazimmoja mjini Unguja.

Alieleza kuwa hadi sasa tayari wana kesi zisizopungua 41 za wahusika mbalimbali katika utoaji wa huduma za afya huku tatu kati ya kesi hizo tayari zimeshaanza kusikilizwa na nyingine zipo kwenye majadiliano zaidi.

Zanzibarleo

Share: