Habari

Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya 1984

DECEMBER 4, 2017 BY ZANZIBARIYETU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA SHUGHULI ZA MKUTANO WA NANE WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOANZA TAREHE 6 DISEMBA, 2017

Mkutano wa Nane wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 6 Disemba, 2017, saa 3:00 asubuhi.

SHUGHULI ZITAKAZOFANYIKA.

Shughuli za Mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-

Maswali na Majibu.
Maswali 113 yameratibiwa kwa ajili ya kujibiwa kwenye Mkutano huu.

Miswada ya Sheria
Miswada ya Sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa Septemba – Oktoba, 2017 itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika Mkutano huu wa Nane.

Miswada yenyewe ni:-

Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar na Kuweka Vifungu vya Usajili na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.

Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati Pamoja na Kuwezesha Ushajihishaji na Uendelezaji wa Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.

Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na Kuweka Masharti Bora Ndani Yake.

Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya 1984 na Kutunga Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2017 na Masuala Mengine Yanayohusiana Nayo.

Ripoti ya Utekelezaji wa kazi za Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hoja Binafasi ya Mjumbe kuhusu Kuweka Miundombinu bora kwa watu wenye Ulemavu katika majengo, barabara, makaazi, maeneo ya kupumzikia na maeneo mengine.

Maombi (Petition) ya wananchi wa Kisakasaka Zanzibar kuhusu namna wanavyoweza kufaidika kutokana na machinjio ya wanyama yaliyopo kwenye maeneo yao.

Raya Issa Msellem
Katibu

Baraza la Wawakilishi
Zanzibar

Tarehe 4 Disemba, 2017

Share: