Habari

Mtoto wa miaka 3 afariki dunia baada kutiwa kisimani Zanzibar

June 12, 2018

Mtoto wa kike (Thuletha Kondo Khamis ) anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 amefariki dunia kwa madai ya kuwa ametupwa na mtu mmoja ambae alijaribu kumuiba na kukimbia nae.

Habari kamili ya tukio hili tutakuwekea hapo baadae , hivi sasa tunakuhabarisha tu kwa ufupi jinsi tukio lilivyotokea.

Ni tukio la jana majira ya saa 3 za asubuhi huko Tomondo Unguja.

Mashuhuda wamesema kuwa , kulikua na watoto wawili mtu na kakaake waliyokua wakicheza nje ya nyumba yao, ghafla akatokea mwanamke mmoja aliyevalia vazi la baibui , shungi na nikabu, alimtaka mtoto mmoja kati ya hao amtume dukani , lakini watoto hao walisema watakwenda wote dukani na wakati wanaelekea dukani , mwanamke huyo nae aliwafuata kisha alimchukua mmoja kati ya watoto hao ambae ni mdogo na kutokomea nae.

Baada ya kumchukua alionekana mama huyo akikimbia nae na waliyokuwepo walijaribu kupiga kelele kumnadia mwizi lakini aliwahi kukimbia na mtoto huyo pasi na kuonekana

Muda mrefu ulipita bila ya mtoto huyo kuonekana , na harakati za kumtafuta zilifanyika hadi kukaja taarifa kuwa ndani ya kisima cha maji kuna mtoto na askari wa kikosi cha uwokozi walikuja na kushirikiana na wananchi kumtoa mtoto huyo, alikua ameshafariki dunia.

Hadi sasa mtuhumiwa hajapatikana na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kumsaka na hatua nyengine ili sheria ichukue mkondo wake

Mtoto huyo amezikwa jana majira ya saa 12 jioni Mwanakwere.

Usikose kufatilia mtandao wetu tutakuweka habari kwa ukamilifu wake hapo baadae

Pembatoday

Share: