Habari

MUUNGANO NDIO ADUI WA ZANZIBAR

na Mzee Kondo

Tunaposema hatutaki MUUNGANO wengine wanafurahi,wanakebehi,wanatukana, wanacheka na kusema maneno ya tashtiti ili wakidhi kiu yao ya kudharau mawazo ya wenzao,hata kama wao wananufaika na huu muungano, sio sehemu yao kuwasemea/kuwatukana wengine wanao teseka nao.

Sehemu kubwa au karibu asilimia zaidi ya tisini ya Wazanzibari ni masikini sana,kundi hili lina watu wa mlo mmoja mpaka miwili tu kwa siku,humu mna pia na wale ambao ni lazima wagaiwe mlo mmoja bure kwa siku na ndugu,jamaa/marafiki au majirani kwa kuwa wao binafsi hawana uwezo wa mlo huo.

Sasa unapoibana na kuilazimisha Zanzibar kulipa gharama hizi karibu mara mbili na nusu yake, yaani kumi kwa tatu, kuliko wanavyo tozwa Uganda,Zambia au Congo ambao hawa kufanya kosa la kuungana na Tanganyika, ina maana sisi tumefanya kosa kubwa kuungana na ndugu zetu hawa, kwani ingelikuwa tumebakia kuwa nchi huru kama tulivyokuwa kabla huu muungano,basi na sisi tungekuwa tuna ‘qualify’ kupewa bei ya nchi zilizo huru kama hao majirani zetu nilio wataja,lakini kwa kuwa sisi ni Koloni lao,ndio maana tuna tozwa kama desturi ya koloni linavyotakiwa kutozwa huu ndio ukweli.

Upuuzi kama huu eti nao umebatizwa jina la KERO,ambazo miaka hamsini na nne sasa bado tunapita tukiunda tume na wizara kuzishughulikia,hatuwezi kumkabili mkoloni kwa sababu mkoloni ndie anae tuchagulia nani awe Gavana hapa sio rais.

Juzi baada ya futari na kumaliza kusali sala zote za siku hiyo,nilikaa katika mkeka wangu mbovu huku nikitafakari mengi ya maisha na moja kubwa lililo kuwa linanisumbua sana ilikuwa najiuliza,hivi nani bora katika watawala au wakoloni baina ya yule mweupe na huyu mweusi?

Nikisema mweupe nina maanisha awe Muingereza,Mreno,Mfaransa,Muarabu,Mjerumani,Mdachi au Mlatino au huyu Mweusi yaani Msukuma,Mkwere,Mzanamo,Mmakonde au Mzaramu,baada ya tafakuri ya muda nikagundua hakuna aliye na afadhali wote wamenyonya ziwa moja, tofauti baba tu yaani rangi.

Sisi Wazanzibari tunaoteseka na kutawaliwa huku madhila yake hayana kipimo,ugumu wa maisha tulio nao ni wa kujitakia kwa sababu sisi ni kidogo,mkoloni ana hiari aiendeleze na kutatua matatizo ya Kigoma kwao,kwa kununua sukari Brazil, kuliko kununua Sukari ya Zanzibar,sasa hawa watu tunawaita ndugu zetu kwa kuwa tumefanana sura au?

Huu Muungano mzee Karume angelikuwa hai angelikwisha uvunja zamani sana,ndio maana walihusika katika mauwaji yake.

Sisi Wazanzibari tufike mahali tuache maneno ya kulalamika bali tutafute mbinu ya kumkabili mkoloni na vibaraka wake kwa kuwashughulikia,hapa sitaki kutafuna maneno hawa ni maadui ni lazima tuwaondoe ili tuvihami vizazi vyetu, kwa sababu sisi ndio wamesha tunakamisha tayari,wasaliti huwa wana uwawa katika nchi za wenzetu.

Nafahamu kwa imani tuliyo nayo katika dini na utu wetu ndio inayotumika kutupoza ili tutawaliwe milele,sasa kama tunaogopa na hatutaki kufa basi pepo tutaisikia tu.

MUUNGANO NDIO ADUI WA VISIWA HIVI.

Share: