Habari

MZALENDO NET WAJIBIWA MAKAVU LIVE KWA UONGO JUU YA VITA YA CUF

 
MZALENDO NET NA UPOTOSHAJI ULIOJAA DHANA OVU DHIDI YA IKULU.

Na David Maphone.

IKULU HAINA SABABU NA WALA HAIJAPATA KUSHIRIKI KATIKA KATIKA MGOGORO HUU.

Kwa maelezo yote niliosoma kwenye maandishi ya Mtandao huu wa MZALENDO NET unaopata nguvu kwa kusambazwa andishi lake na wafuasi wa chadema na Maalim Sefu inaonyesha Mwandishi/Waandishi wa maelezo hayo hawajui chanzo cha MGOGORO au wanapotosha KUSUDI.

NINI CHANZO CHA MOGOGORO ?

Chanzo harisi cha mgogoro huu ni kufeli kwa mpango wa Maalim sefu kutaka KUVUNJA muungano kwa kutumia mchakato wa Katiba mpyawakati wa kupeleka maoni ya chama kwenye tume ya Jaji warrioba.
MWENYEKITI alisimamia serikali tatu kama ambavyo katiba ya cuf imekuwa ikisema.
KATIBU akisimamia serikali ya NKATABA kuipatia zanzibar mamlaka kamili na muungano kuvunjika .
Maalim sefu alichukua maoni yake ya NKATABA bila kushirikisha chama yaani vikao na kupeleka kwa Jaji warrioba na kusema ndio maoni ya Baraza kuu.

Prof Lipumba alichukua maoni ya Baraza kuu ya serikali TATU na kupeleka kwa Jaji warrioba na kukuta Maalim sefu kishapeleka maoni yake na kusema ni maaoni ya chama.
JAJI WARRIOBA AHOJI

Nimepokea maoni ya Chama kimoja mawili tofauti moja serikali ya NKATABA kaleta KATIBU na mengine ni serikali TATU umeleta wewe MWENYEKITI yapi sasa yatakuwa ni maoni sahihi ya chama?

Prof Lipumba alimwambia Jaji warrioba asome katiba ya Cuf Ibara ya 91(a) na (b) zinazosema mwenyekiti ndio Kiongozi mkuu wa Chama na ndio msemaji mkuu wa chama.

Baada ya kupitia katiba ya Cuf Jaji Warrioba aliyatuba maoni ya Maalim Sefu HAPO NDIPO CHUKI ZA MZEE HUYU ZILIPOANZA.

NGOJA TURUDI KWENYE UONGO WA MZALENDO NET DHIDI YA IKULU.

Kwanza kuhusisha Ikulu na MGOGORO wa Cuf ni mpango mkakati wa wapinzani wa serikali ya mhe Magufuri (RAIS) hasa Mafisadi na waovu mbalimbali kutaka kumdhoofisha kiutendaji.
IKULU hakumwambia Maalim sefu kugoma suluhu na mwenyekiti wake.

IKULU haikumwambia Maalim Sefu Kukaa na barua ya Prof Lipumba kwa miezi( 8 bila kuitisha mkutano mkuu )mpakamuhusika AKATENGUA.

IKULU haikumwambia Maalim Sefu kugoma wito wa kwenda Ofisini anapoitwa na mwenyekiti wake na mpaka leo bado yuko huru kwenda Ofisini akapangiwe kazi na BOSS wake.

MPANGO WA KUMFUKUZA SEFU KURATIBIWA NA IKULU.

Huu tena ni UONGO wa wazi kabisa Mwenyekiti wa chama bado anamtambua KATIBU MKUU ni Maalim sefu na msimamo huu ni wa chama. Na kama utaitishwa mkutano mkuu ni kwa mujibu wa KATIBA na taratibu za chama na maamuzi yatafuata katiba kwa kila mwanachama.

HIVYO maandishi haya yamewekwa kama kinga kwa maalim sefu asichukuliwe hatua kwa kuogopa kwamba IKULU itahusishwa na maamuzi halali ya chama chetu

UONGO WA KUAPISHWA MAALIM SEFU NA ZUIO LA IKULU.

Jambo hili ni la kijinga sana na msemaji lazima awe mjinga kweli kweli !! Lakini kwa sababu mmetaja IKULU mimi sio msemaji wa IKULU lakini kama mtanzania mhe Rais JOHN Pombe MAGUFULI alikwisha toa msimamo wa serikali yake kuhusu uchaguzi wa Zanzibar .
NANUKUU.

“uchaguzi umekwisha zanzibar Rais ni Dkt SHENI mpaka 2020 hakuna uchaguzi mwingine na wengine sio lazima wawe Marais wakauze NYANYA”

Sasa kama JUMUIYA za kimataifa zinakuja kumtoa Dkt SHENI kwa nguvu tunasubiri tuone hayo mapinduzi

MAHAKAMANI NA UONGO WA IKULU KUWEKA NGUVU
Kama kuna eneo Mtandao huu wa MZALENDO NET umeonyesha uongo wa wazi ni kuhusu mahakama na kuhusisha na IKULU.
Kama ni kweli Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kuiendea kesi wanafanya utafiti ni jambo la kupongezwa sana kwa sababu ndio utaratibu bora wa kushinda kesi zinazokuja mbele yao.
Huwezi kuwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Kisha kila kesi wanashindwa na kuisababishia serikali hasara kisa unataka MZALENDO NET na mafiadi wengine wasikushambulie.
KESI ZIMEWEKWA MAPINGAMIZI KWA MAELEKEZO YA IKULU HUU NI UONGO KABISA.
Hivi mwandishi au waandishi wa maelezo haya wanajua sheria kweli na kama hawajui kwanini andishi hili wasilipitishe kwa wanasheria wao.

PINGAMIZI katika kesi (PRELIMINARY OBJECTION) ni jambo la kawaidi na hutumika na anasheria wote huwa ni kipimo bora cha weredi wa mwanasheria katika kuandaa kesi kwa umakini.
Sasa kwa kesi za Maalim Sefu kuweka PINGAMIZI ni swala la kutumwa na IKULU huu ni ujinga na upuuzi wa kiwango cha UROJO.

MASWALI KWA MZALENDO NET.

1 Ni wajumbe wangapi wanaounda kamati ya IKULU kuratibu ushindi mahakamani?
2 Hapo IKULU wanawasiriana na nani tutajie jina lake na majina ya wajumbe wote?
3 Hayo mawasiliano ya IKULU na MAHAKAMA yalifanyinka lini na wapi na wajumbe ni kina nani?
4 MZALENDO NET upo tayari kusibitisha maelezo yako haya katika mahakama za kisheria ?
BADO NAPITIA UPUUZI HUU NINA KUJA KUJIBU HOJA ZOTE STAY TUNE

Imenakiliwa kutoka: http://www.lemutuz.com
Share: