Habari

“NABII” AIBUKA ZANZIBAR!

Kwanza nianze kwa ksema ‘astaghafiru lllah astaghafiru llaah.

Pili niseme kuwa, as I said it again and again, kuwa kila mwenye upuuzi wake anakuja kuufanya hapa Zanzibar.

Kuna mama mmoja amejitokeza na kujitangaza au kusema kuwa yeye ni ‘Nabii” na ameshawahi kufika uwingu wa saba…..na kuona….(almuradi kufru siwezi kusema).

Uzuri wa suala lenyewe limefika ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na baadhi ya ulamaa wamekutana naye mama huyu (Nabii). Ubaya wa suala lenyewe, hawa wooote pamoja na elimu zao, wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya kufru hii. Wamekubali kusalim amri, uislamu wao, imani yao, na kuacha kumuogopa Allah ili wairidhie serikali, na CCM na serikali ya Tanganyika.

Hata hivyo, ofisi ya Mufti imetoa kauli kuwa mama huyu aache kwenda misikitini na kuhubiri.

Pili wametoa fatwa kuwa ahamishwe na kurejeshwa kwao Tanganyika. Suala hilo limepingwa na Immigration na wamedai kuwa yey ni Mtanzania hawezi kuondoshwa kutoka Zanzibar to Bara. Suali linakuja, mbona Kurwa amehamishwa kutoka Zanzibar na kupelekwa Tabora.

Kurwa ana pacha wake anaitwa Dotto, pale kwao Chake Chake, zamani akifanya ATC — shirika la Ndege, then alikuwa anauza duka la michezo. Ahh… hawa pacha baba/mama mmoja: mmoja ni Raia na mmoja si Raia.

OK, huyu mama anayesema kuwa ni Nabii pia Immigration wanasema hawezi kuhamishwa kutoka sehemu moja ya TZ hadi nyengine. Mapalala aliwahi kufanyiwa deportation hiyo. Abdullah Rashid alipokuwa RC Kaskazini Unguja, alizuia watu wa upande mmoja wa kisiwa cha Unguja kwenda kwengine. Deportation act ya ndani ipo, na ndio moja ya sheria mbaya za TZ (draconian law, na hata report ya Nyalali ilipendekeza ifutwe).

Turudi kwa ‘Nabii” wetu. Huyu Immingration wanasema hawezi kuwa deportated just kwa sababu amekuja kuwadhalilisha na kuwatusi wazanzibari na uislamu na serikali inamtetea kwa hali zote. Hii ndio hali inayotukabil jamani, na kama hatutaki kuamka basi hatuamki tena. Huyu mama ni murtad – lakini kaimu katibu wa Mufti anaitwa Jongo anamtetea just kwa sababu ni mtu wa kwao KIMBIJI (mndengereko mwenzake); ahhhh…. ametoka Soraga amekuja Jongo — hao kwa hao.

Huyu mama amekuja (kahba mmoja tu) amekuja na kujingazia kuwa yeye ni “nabii’. na Tumekubali. Tumeambiwa katika quran tukufu kuwa Mtume Muhammad SAW ndiye wa mwisho, tunahoji nini au tunataka nini zaidi ya hilo, leo aje janajike pumbavu kama hili kahba la kupepea asema yeye ni ‘nabii’ na sisi tumekaa tunakodoa macho tu.

Jana nimezungumza na sheikh mmoja — yeye anasema ‘ah huyu anatafuta mume tu’. Huyu ni sheikh mjinga na niligombana naye kidole machoni kuwa mimi niko serious, yeye ananiletea mambo ya kipumbavu.

Angalia: mama huyu aliwahi kuzungumza na rafiki yangu mmoja,miaka miwili iliyopita; alisema ana miaka 40; kuna msikiti ameingia jana pia amesema kuwa ana miaka 40. Ina maana ‘nabii’ huyu hakui miaka yake?

Tuendelee kuwakamata UAMSHO, na tuwaenzi ‘manabii’ kutoka Mkuranga na Kimbiji

 

Share: