Habari

Nani ataenda kupiga kura hio tarehe 20

Zanzibar ni CUF na CUF ni Zanzibar kwa maana asilimia 95 ya waZanzibari ni wafuasi wa Chama cha CUF na CUF wamegomea kushiriki uchaguzi usio na kichwa wala miguu ni nani huyo atakae kwenda kwenye kituo na kupiga kura ?

Naona kuna aibu nyingine inainyemelea CCM kutangaza matangazo ya uongo uliopindukia ,kiukweli uchaguzi mkuu uliomalizika punde miezi michache mbali ya kubebwa kiundani CCM haikupata hata asilimia tano ya ushindi ,CUF iliishinda CCM kwa mbali sana sana ,kushindwa ambako waameingiwa na butwaa na kufanya mambo yasiyokubalika wala yasio elekea ni aibu tosha ,wameufuta uchaguzi kwa kuwa tu wameshindwa ,jambo ambalo hawalioni au wamejitia upofu ni hao watakaoifanya CCM ishinde watatoka wapi maana hawashiriki uchaguzi au hawaendi kupiga kura.
Jecha hawezi wa hana uchaguzi zaidi ya kutaka kuvunga vunga aitangaze CCm imeshinda sasa hesabu na nambari atazitowa wapi ? Au anategemea hivyo vyama vitakavyoshiriki ambavyo havina wanachama hata mmoja Zanzibar zaidi ya wagombea uraisi au wanategemea polisi na majeshi kwenda kuwapigia kura ? Kwa maana hiyo tutegemee malori ya vikosi vya SMZ kusafirisha wapiga kura kutoka kituo hadi kituo ?

Share: