Habari

Ni nini kinachoitafuna Zanzibar ndani ya NECTA?

Kwa masikitiko makubwa naomba kuwauliza wenzetu wa Zanzibar swali ambalo kwa kweli limekuwa likinitatiza miaka mingi sana. Nalo ni udhaifu mkubwa sana wa taaluma ya Zanzibar ndani ya baraza la mitihani NECTA.

Cha ajabu kabisa ni kuwa, wakati Zanzibar hiyo ikiwa hoi mbele ya NECTA, wapo Wazanzibar wengi sana ambao ni wana vipaji vya hali ya juu sana mfano kina Mohamed Gharib Bilal na wengine wengi sana. Hawa wana vichwa vilivyojaa vipaji.

Katika matokeo ya kidato cha sita ACSEE-2016 Unguja pekee imetoa shule saba kati ya kumi za mwisho, nini tatizo?

Siongelei kuhusu swala la ghafla bin vuu shule kongwe za serikali za vipaji kurudi kwenye chati maana hilo linahitaji uchambuzi wake. Ni wachache watakaoamini kuwa shule zote kongwe za serikali za vipaji kurudi “top ten” kwa kishindo kumetokana na jitihada binafsi za wanafunzi. Shule zote nne? Hapana! Hili tutakuja kulichambua baadaye! Kwanza niwaulize hawa watani zetu, nini tena kimewapata?

Shule 10 zilizofanya vibaya:

1.Mpendae-Unguja
2.Ben Bella-Unguja
3.Tumekuja-Unguja
4.Green Bird Boys-Kilimanjaro
5.Jang’ombe-Unguja
6.Kiembe Samaki-Unguja
7.Tanzania Adventist-Arusha
8.Al- Ishan Girls-Unguja
9.Azania-Dar es Salaam
10.Lumumba-Unguja

Imenakiliwa kutoka kwa G Sam (jamiiforums)

Share: