Habari

NJAMA ZA KUTEKA ZAVUJA

Habari zilizopatikana kutoka kwenye Kikao kilichofanyika Michungwamiwili kilichohudhuriwa na Waziri wa SMZ Haji Omar Kheri, Thiney Juma, Kiongozi wa UMAWA, Kiongozi wa KVZ na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi kimeazimia kumteka au kumpoteza kabisa Kamanda Mkuu wa CUF na Viongozi wengine WAANDAMIZI wa Chama hicho. Tayari picha za wahusika zimeshatumwa maeneo tofauti kukamilisha mkakati huo.

Matokeo ya aina hii yamekuwa ya kawaida kwa upande wa Tanzania Bara katika siku za karibuni ingawa Zanzibar inasifika kwa matokeo hayo ya kinyama na kikatili. Mwaka jana Mhe. Ali Juma (Aliuekuwa Mkurugenzi wa Habari wa Wilaya ya Magharibi “A” CUF) alitekwa nyumbani kwake na kupigwa, kuchomwachomwa midomo ya Bunduki sehem mbali mbali za mwili na baadae kutupwa na kupoteza uhai akiwa spitali ya Mnazi Mmoja.

Katika Hali ya kufadhaisha na kusikitisha ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, baadhi ya mawakala wa CUF walitekwa kutoka majumbani mwao: kupigwa, kuteswa na kutelekeza maeneo tofauti ya Zanzibar. Pia Wanawake zaidi ya wanne wa CUF wametekwa na kufanyiwa udhalilishaji wa kupitiliza katika maeneo tofauti Khususan wilaya ya Magharibi “B” Zanzibar.

Wazanzibari bado hawajasahau kutekwa kwa baadhi ya waandishi na kudhalilishwa, kuchomwa Moto vituo vya redio, kufatwa kwa waandishi katika vituo vya kazi matokeo ambayo yalizua taharuki kubwa Zanzibar bila ya kusahau mauaji ya kikatili ya mwaka 2001. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Michungwamiwili matokeo haya huenda yakashamiri katika Kisiwa Cha Unguja na Pemba na kushuhudia baadhi ya Viongozi wa CUF kupotezwa kama njia ya kukihujumu Chama Cha Wananchi CUF, imeelezwa kwamba mikakati ya Kuteka watu na kuwapoteza, kuvamia Ofisi za Chama Mtendeni, Kupelekwa kwa Lipumba kisiwani Pemba ni mikakati inasimamiwa na Balozi Seif Ali Iddi na kamati yake ya Siri ambayo tayari wanzanzibari wameshaijua na wanaifaatilia kwa umakaini mkubwa.

Kamati hiyo ya Siri iliyoundwa kinyume na utaratibu wa kiitifaki wa TISS, ambayo pia ina baraka zote kutoka kwa baadhi ya watu wazito kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Jasusi maarufu aliyetumika kuongozi idara ya TISS kipindi Cha mfumo wa Chama kimoja; Jasusi mstaafu Dokta Hassy Kitine aliyebobea katika misingi ya chuki na ukatili dhidi ya wanamageuzi ambae pia hataki kuiona Zanzibar inapata mabadiliko. Baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo ni Hamad Rashid (Waziri wa Afya na Jasusi wa muda mrefu), Abdallah Khamis (Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji) , Haji Omar Kheri (Waziri wa Vikosi vya SmZ), Mohd Juma Ame (Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vitambulisho vya ZAN ID) na Rashid Simai MSARAKA.

Haya na mengine yanafanywa kwa lengo moja tu: KUVURUGA AMANI NA UTULIVU ULIOPO ZANZIBAR licha ya Juhudi kubwa zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Viongozi wa CUF kuhakikisha wanadai Haki za Wananchi ikiwemo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 kwa njia za amani.

Na: Juma Mrisho MAPWEZA wa Zanzibar

Tagsslider
Share: