Habari

Ofisi ya CUF Zanzibar yateketea na moto

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametembelea ofisi ya Chama hicho jimbo la Dimani.

Maalim Seif amefanya ziara hio baada ya watu wasiojulikana juzi Usiku kuichoma moto ofisi hio na kuteketeza vitu vyote vilivokuwemo ndani yake.

Mara baada ya ukaguzi huo Maalim Seif akiongea na vyombo vya habari alisema kitendo hicho ni cha kulaaniwa na hakipaswi kufanyika katika kipindi kama hichi.

Alisema matendo ya namna hii yalikua yakifanyika katika zama za siasa za Chuki visiwani Zanzibar ambapo kwa sasa zimeondoshwa baada ya uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Aidha Maalim Seif alitoa wito kwa wanachama wa Chama cha CUF kutolipiza kisasi kwani kufanya hivo kutasababisha uwepo wa uchafuzi wa Amani.

Tagsslider
Share: