Habari

Polisi Zanzibar yamshikilia Mkurugenzi Juvicuf kwa ripoti ya ubaguzi wa ajira

Tokea Jana usiku, Polisi Zanzibar inamshikilia Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo vikuu wa Jumuiya ya Vijana CUF – Juvicuf, Bw Mohamed.

Sasa hivi yupo kutuoni Madema kufanya mahojiano na maafisa wa upelelezi juu ya tuhuma alizopewa juu ya report yake aliyoitowa hivi karibuni kushutumu mpango mzima wa uajiri unavyokwenda hapa Zanzibar.

Pia anadaiwa kutoa maneno yasiyopendeza kwa Serikali ya Zanzibar.

Tokea Jana mchana hali ya usalama Zanzibar ilikuwa imedorora. Kulikuwa na taarifa za watu zaidi ya 40 wamepigwa na watu wasiojuilikana huko maeneo ya Tunguu.

Huu ni mkakati maalum wa Serikali ya Tanganyika kuleta hali ya utata na njia ya kuwadhibiti Wazanzibar wasiendelee kudai haki za nchi yao.

Share: