Habari

Rasimu ya Katiba Mpya: 11-7=14

Jana nimeisoma rasimu yote ya katiba mpya, inayoitwa ‘first draft’. Mimi ninaitazama kama vile ni ‘final version’; na ninathubutu kusema kuwa au kuuliza kweli hii rasimu imeandikwa imeandikwa na tume ya Warioba au imechukuliwa pahala ambapo tayari ilikuwa imeshaandikwa, kama vile ‘cut and paste’ na kimetumika kivuli cha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kama kivuli tu. Mimi siamini kama mawazo haya kweli yameandikwa na mtu kama Salim Ahmeid Salim, Warioba, Ally Saleh, and others. Hii hata motto/mwanafunzi wa darasa la 4 anawez akusema maneno kama haya. In short, maneno yaliyoandikwa hayana mantiki, na imepoteza merit za hao wajumbe. aibu, kinyaa, uoza, uchafu mtupu — taka taka.

Sasa tuanze kuchambua: nilivyofahamu mimi ni kuwa rasimu hii imejidai kutoa mambo 11 ya awali ya Muungano na kuyaunganisha kuwa saba, that means, kila item moja ya 1964, imefanywa kuwa mbili, eg: ‘Uraia na Uhamiaji’ etc. hesabu yao imekuwa ni sawa na mambo 11-7, utapata nne, lakini jawabu yao imekuwa 14.

Hii maana yake INAIFUTA ZANZIBAR MOJA KWA MOJA KATIKA RAMANI YA DUNIA, NA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KIWETE MAISHA NDANI YA UTAWALA WA TANZANIA/TANGANYIKA.

Alichokifanya warioba ni kama vile ‘he zipped files, all files’ na amelifanya kuwa moja, ‘two in one’.

Lakini jamani mimi nilisema ukumbi huu kuwa hata siku moja Warioba hatoitendea haki Zanzibar, na kwa sababu kuwa yeye kwanza ni muumini wa serikali moja, lakini pia, anasadikiwa sana kuwa yeye ni group la akina Njelu Kasaka, G-55, ambaye alikuwa anataka serikali ya Tanganyika irudi ili wapate kuidhuru Zanzibar zaidi. Ninachokijua ni kuwa 90% ya mawazo yaliyoandikwa katika rasimu hii, ni sawa sawa na yale yaliyomo katika document ile ya G-55. Mimi sinayo tena, naomba tuitafute. Na kama sikweli mje mnisute!

Nilisema hapa mzalendo — kuwa ukiona kiongozi wa Tanganyika ameunda tume au kamati yeyote ile na wjaumbe wa Zanzibar wakawa 50-50 inakuwa wanataka kufanya jambo kubwa la kuidhuru Zanzibar zaidi. Na hii nilisema na sasa ina-prove my point!

– Jamani ale wajumbe wa Zaanzibar ndani ya tum hii, ndio kweli wameridhika na haya? Yaani kuihujumu Zanzibar, kuifuta Zanzibar kabisa kabisa katika ramani ya dunia, tujue kuwa hii sio ‘draft’ — ila hii ni final document na mtakuja kunikumbuka.

– What to do?
1. Wale wajumbe wa Zanzibar waanze kujitoa ndani ya tume ile kwa maana kuwa ‘it doesn’t reflect views of majority Zanzibaris’

2. Wabunge wa Zanzibar (kama watakuwa na akili) waikatae rasimu hii itapokwenda Bungeni, na wabunge wa Zanzibar bado wanayo theluthi mbili ya kura mle bungeni, hii ndio last shot to hit, lau kama akina Sanya wanataka kujadili mambo ya mashoga tu haya. Tutazama sote. Waoa amali yao kubwa Bungeni wanajadili mabo ya kipuuzi na kupiga miayo tu.

3. Wajumbe wa BLW, tutawaona hapa: muikatae rasimu hii au kama mtaletewa kama ‘memo au taarifa’ na mtaipokea, na uzuzu wenu haya. Tutazama sote, na baadaye akina Othman waje pale ukumbi wa Bwawani au taasisi wapige makelele yao ya kipuuzi na huku wazanzibari wanawafurahi kwa uzuzu wetu.

4. Itapokuja uraiani, piga NO katika referendum (najua hili litakuwa gumu kigodo kwa sasa) kwa sababu tayari kuna kambi nyingi kwa baadhi ya majimbo hapa Zanzibar kwa ajili ya kuja kupiga kura za bandia. Mmojawapo ni xxxxx na jimbo yyyy ambaye yeye hujifanya anatetea sana maslahi ya Zanzibar against union akia baraza la wawakilishi.

Whatever trash aliyotuletea Warioba na wenzake, bado tunayo chance ya kurekebisha mambo kama tutakuwa wakwlei, smart, na kutumia akili — na kama tutapata support ya viongozi wetu – otherwise, tunazidi kuyoyoma.

Akina Awadhg, Ally Saleh, Muhammed Yussuf etc — hivi kweli hamkuona urojo (uharo) huu ukaindikwa na nyie mmeukubali?

Hebu nielezeni kimantiki kweli sisi kama Zanzibar Revenue Board (ZRB) kwlei itakuwepo wakati ushuru ni sehemu ya federal govt, na je, zile pesa/makusnayo ya kodi ya madini yatakuwa yetu, yao, au sote??? just example? Kweli ZRB itakuwepo?

Mnakumbuka last week nilisema kuwa mtapewa serikali tatu, na Zanzibar itabaki kama -ki-idara tu ndani ya union government, je. mmeona sasa?

– Je, sasa mmeona kuwa makongamano ya kipuuzi kama yale ya Bwawani kuwa hayana maana wala tikji ila ni sherehe na mradi wa watu Fulani ule wa kutafuta pesa? Pale ni uitapeli tu jamani. Hizo ideas ninazokupa kama mtazifuata ndio njia sahihi. Othman Massoud jana nimekuona pale kwenye viwanja, na nimemuona Maalim Seif and others — kweli Othman utaikubali uoza huu, ambaye hata kama mimi niliyekuwa si lawyer, basi ninaweza kuandika INSHA ile ya darasa la tano au nne, its’a primary school composition. Billions of shs zimetumika na results ndio ile. Nina wasiwasi/shaka document ile ilikuwa imeshaandikwa jamaa wamekwenda kuibeba tu pahala ‘cut and paste’ and zipped all files. Hebu tuutafute warka wa G-55 ule wa akina Njelu Kasaka, hauna tofauti na huu, takriban 90% contents ndio hiyo hiyo. Kweli 11-7 = 14 (erase Zanzibar from the world map).

Share: