Habari

Safari ni hatua, huenda tukafika

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akichukua chakula wakati wa Futari iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ,katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar leo,pamoja na wananchi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo

Mwezi mtukufu wa Ramadhani na barka zake. Tabia za waja kikamilifu zinabadilika. Jee ni kwa heshma ya mwezi huu mtukufu au ni kuonengezeka imani nyoyoni miongoni mwa Waislam.

Picha hii imenifanya nijiulize, sasa viongozi wetu wanaelekea kufahamu kuwa uongozi ni kuwatumikia wananchi. Unapoitwa Rais, siyo kuwa umetiwa kikutini, laa, bali ni kuongezeka kwa majukumu yako.

Hivi ndio viongozi wanavyotakiwa kuwa mfano wa jamii yao. Ikiwa wao ni watumishi wa watu inapendeza wanapoonekana wakiwa mstari wa mbele kuwadumikia. Badala ya kukaa na kujifanya mabwana.

Leo Dr Shein anapanga foleni ya kuchukuwa chakula, jee hayo si maajabu. Safari ni khatwa.

Share: