Habari

Salama Aboud Twalib amevunja “Code of Cunduct” za cheo chake

Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Salama Aboud Talib amevunja “Code of Cunduct” kwa kitendo chake cha kwenda kumchukulia dhamana mshukiwa wa makosa ya jinai Hassan Aboud Talib.

Mshukiwa Hassan alikamatwa na jeshi la polisi kufuatia madai ya kiudhalilishaji ya jinai ambayo ni zaidi kuliko hata hiyo sheria ya ubakaji, kwani kitendo cha kumlewesha au kutumia dawa kisha kumuingilia kwa nguvu ni mkusanyiko wa makosa ya kisheria kadhaa kwa pamoja.

Waziri Salama amevunja code of cunduct kwa njia mbili, moja; Kutumia cheo chake kama Waziri kwenda kumchukulia dhamana ili awe nje mshukiwa. Pili, kutumia cheo chake kuleta conflict of interest, kwa vile Hassan ni ndugu yake hivyo ametumia madaraka yake vibaya kwa “UMIMI” au “KUJUWANA”.

Sikushangazwa kusikia Wawakilishi wakipaza sauti zao wakihoji kwa Waziri Salama na kile alichokifanya akijuwa fika kuwa huko ni kwenda kinyume na misingi ya utawala bora. Waziri Salama pia hii sio mara ya kwanza kushutumiwa kwa kile kinachoitwa “arrogant” wa madaraka, kwani amekuwa akishutumiwa kutumia madaraka na nafasi aliyopewa kwa kibri na majivuno kama vile limbukeni. Siku za hivi karibuni zililetwa taarifa na kupelekewa Rais Dr Ali Mohamed Shein.

Ikumbukwe mara baada ya kuteuliwa kuongoza nafasi nyeti kama hizi, viongozi hupewa mafunzo ya hali ya juu yenye kugharimu kiasi kikubwa cha fedha za wananchi. Miongoni mwa mafunzo kama kutunza siri za serikali, code of cunduct za uwaziri, na guides nyeninezo ili kuwajenga uwezo na uwelewa zaidi. Kinachopatikaba ni utumiaji mchafu wa madaraka kama vile watu waliokuwa hawaja elimika.

Katika kikao cha Baraza, Wawakilishi wameibana serikali kutokana na matendo ya Waziri Salama kwa kitendo chake cha kumchukulia dhamana mshukiwa. Waziri Mohamed Aboud Mohamed amesema “Jitihada ya serikali kuhakikisha wahalifu wanachukuliwa hatua kali ili kudhibiti makosa mbalimbali yanayotokea”.

Kuhusu suala la kufanya utetezi kwa mtu aliyefanya makosa ya jinai na kubaka, Waziri Mohamed amesema: “sheria ni msumeno, hakuna aliye juu ya sheria… yoyote atakayekwenda kinyume na sheria hatua za kisheria zitachukuliwa na adhabu kali dhidi yake zitamkuta.” Waziri Mohamed ametowa wito kwa viongozi na wananchi wote kutii sheria kwani kuna mpango maalumu unaoandaliwa kukabiliana na wale wote wanaovunja Sheria.

Wawakilishi wameitaka serikali kuchukuwa hatua kwa Wiziri wa wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib kwa kufanya utetezi na kwenda kumchukulia dhamana mshukiwa wa uhalifu.

Mwakilishi Ali Sleiman Ali amesema “juu ya kadhia hii ya kudhalilishwa watoto wetu na wanawake nilishindwa kuendelea, nilitokwa na machozi mpaka pressure kunipanda”. Mwakilishi Ali Sleiman alitaka kujuwa hatua za serikali itakazo chukuwa kwa Waziri Salama kwa hatua yake ya kwenda kufanya utetezi wa mshukiwa.

Sisi wananchi ambao hatuko Barazani pia tunaihoji serikali ni hatua gani itachukuwa kwa Waziri Salama juu ya hoja mbili nilizozitaja hapo juu, mbazo ni kuvvunja code of conduct na conflict of interest .

Niimani yangu kwa Rais Dr Shein hili hatolifumbia macho, atafanya kwa maslahi ya jamii na serikali yake inayosimamia misingi ya uwajibikaji na utawala bora.

Share: