Habari

Samiah Suluhu Umeteleza au Umekusudia?

Samiah Suluhu umewatangazia wajumbe wa Bunge Maalum kuwa kutakuwa na sala ya kuliombea dua Bunge maalum, kilichonishangaza ni kuwataka Wakristo – UKIWEMO WEWE – kushiriki dua hiyo. Kwa kukunukuu umesema kuwa Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga “atakuja kusali katika kanisa la hapa bungeni saa 7 mchana kwa lengo la kuliombea Bunge Maalumu…Wakristo wote tunaombwa kujumuika katika sala hii,”

Habari zaidi ipitie hapa chini:

Dodoma.

Wakati viongozi wa dini wakipaza sauti kutaka maoni ya wananchi kuheshimiwa, Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma, leo litaendesha sala maalumu ya kuliombea Bunge Maalumu la Katiba.

Ibada hiyo ambayo itafanyika saa 7 mchana katika kanisa lililopo ndani ya maeneo ya Bunge, itaendeshwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga.

Kuendeshwa kwa ibada hiyo maalumu, kulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samiah Suluhu Hassan.

“Atakuja kusali katika kanisa la hapa bungeni saa 7 mchana kwa lengo la kuliombea Bunge Maalumu…Wakristo wote tunaombwa kujumuika katika sala hii,” alisema.

Ibada hiyo inaendeshwa zikiwa zimepita siku chache tu baada ya Maaskofu 32 wa kanisa hilo kutoa waraka maalumu wa Pasaka kwa wajumbe wa Bunge hilo wakiwataka kuheshimu maoni ya wananchi.

Maaskofu hao walisema ili kupata Katiba bora, wajumbe wanapaswa kuheshimu kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuitumia kama ilivyokusudiwa na sheria.

Na Daniel Mjema, Mwananchi

Posted Alhamisi,Aprili24 2014 saa 24:0 AM

Share: