Habari

SASA WALIOSALITI MAPINDUZI YA 1964 WATAKIWA KUTOSWA KWA KUKIKAZWA CHAMA CHA MAPINDUZI

Kumezuka hisia kali sasa kutoka kwa wahafidhina wa Chama Cha Mapinduzi (Afro Shirazi Asili) kuwa wale wote waliozembea kuwajibika ipasavyo kabla ya kufanyika uchaguzi na kukikwaza Chama Cha Mapinduzi kwa kukifikisha hapa kilipo sasa watoswe.

Imedaiwa Balozi Seif Ali Idd na Waziri Mohamed Aboud wameshindwa kuwajibika kwani Tume ya Uchaguzi ipo chini ya Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wamezembea katika maandalizi yake na kukikwanza Chama Cha Mapinduzi. leo tupo katika mtihani mgumu kuliko yote iliowahi kuimkumba nchi hii tangu mapinduzi ya 1964 sasa umefika wakati watoswe, kwani hawakuwepo kujali maslahi ya chama walikuwepo kujali maslahi yao binafsi.

Aidha pia “Right Handman” wa Dr. Shein ambao walikuwa wapambe bila kujali kuwa walikuwa na wajibu wa kusaidia mikakati ya CCM kufanikisha kushinda uchaguzi sasa na wao pia watoswe madai hayo yameorodhesha wapambe wa Dr. Shen wanaopaswa kutoswa na chama kwa kuyasaliti mapinduzi ya mwaka 1964 ni

Pandu Ameir Kificho
Haji Omar Kheir
Ramadhan Abdallah Shaaban
Omari Yussuf Mzee na
Ali Vuai

Kwamba wamekikwanza Chama Cha Mapinduzi na kukifikisha hapa kilipo, chama kimetumia pesa nyingi kugharamia kampeni na kwamba kwa kutokuwa na majimbo kwa maana ya wapiga kura wameshindwa kuwa na mbinu za kisasa katika ushindani wa siasa ya vyama vyingi walidai wakereketwa hao kwamba hata mwaka 1957 wakati Afro Shirazi inapigania uhuru tulifanya vyema katika uchaguzi kuliko sasa ambapo walikuwa na kila uwezo kwa kukiletea ushindi CCM usio na kelele. Waondoke sasa walidai waasisi hao wa CCM.

Aidha madai hao hayakumuacha nyuma Mkurugenzi wa Usalama Zanzibar kwamba alizembea yakatokea yaliotokea bila ya serikali kuwa na taarifa nayo na kushitukizwa na mkutano wa waaandishi wa habari na chama ca CUF na yeye pia Afro Shirazi hao asili walitaka atoswe sasa kwa maana madaraka kwa miaka 15 yamemlevya na kupata kiburi cha ajabu.
12182800_1059924904017645_3831575736239815012_o

Share: