AudioHabari

Sauti – Masheikh Pemba wampa makavu Mufti

SHEKH KABI ABANWA KOO PEMBA.

Ni baada ya kutaka kuwaombea wafuasi wa CCM wasifanyiwe mgomo. Aambiwa kama angekwenda Gongo na wenziwe wote wangeachiwa ukumbi mtupu. Abanwa kuhusu mashekhe wa UAMSHO. Masheikh wasema anakoroga kinyesi halafu anategemea kuskia harufu mzuri. Aambiwa pasi na Shein kuirejesha haki aliodhulum nchi haiwezi kua na amani.

Kweli CCM hawamjui Mungu mpaka pale waone wameinamiwa. Mufti mkuu wa Zanzibar Shkh. Saleh juzi alifanya kikao na masheikh wa Pemba ambapo kikao hicho kililenga kuwataka masheikh hao wasaidie katika kuiweka jamii pamoja na kuwataka wasitishe zoezi la mgomo linaloendelea kisiwani huko tangia kurejewa kwa uchaguzi wa March 20.

Wakati Sheikh Saleh na ujumbe wake aliokwenda nao wakiwataka masheikh hao kufanya hivyo na kuwaremba kwa kila sifa masheikh hao, Masheikh hao wamekuja juu na kusema kua hapawezekani kua na amani na upendo pasi na haki na uadilifu kutendeka.

Mmoja wa masheikh ambao walipata nafasi ya kuchangia alisema na kuhoji kua tunawezaje kuyafikia mafanikio wakati hatujapita katika njia ya mafanikio? Huku akisistiza kua uislam hauangaliwi vipande vipande na kusema kua hatuwezi kuangalia mwisho wa tatizo tu bali pia tunatakiwa kuangaia na chanzo cha tatizo huku akimwambia sheikh Saleh kua asitegemee kukoroga kinyesi halafu akaskia harufu mzuri.

Nae shekh mwengine alisema kua Shein kadhulum na mikono yake inanuka damu na yeye mwenyewe anajua na kumtaka sheikh Saleh amwambie Shein arejeshe haki ya aliowadhulum ndipo amani na upendo utarudi visiwani humo.

Shekh Saleh pia alinasihiwa na kuambiwa kua aya na hadithi alizowatolea masheikh hao aende akawatolee na viongozi wa serikali kama vile Shein, Balozi Seif na Maalim Seif huenda labda na wao kama binadam wakafaham na wakaamua kutenda haki. Huku sheikh mmoja akihoji kwa nini mambo haya waambiwe wao wasiende kuambiwa hao waliosababisha matatizo haya? na kusema kua wao siku zote wanajulikana kipindi cha shida tu na matatizo lakini kukiwa hakuna vitu hivyo na nchi imetulia hawaitwi hata kupewa asante ingawa juhudi za kuituliza nchi kiasi kikubwa huzifanya wao.

Wako masheke pia walimuuliza sheikh Saleh wananchi watafanyaje ikiwa mtu ambaye hana bunduki na uwezo wowote anateswa na kupigwa na kudhalilishwa na Jeshi la POlisi na mazombi bila ya kosa? Je ni haram kwao wao kuchukia? Pia aliulizwa tunawezaje kua na mapenzi ya kushirikiana na watu ambao waliwaweka mashekhe wetu ndani na kujisifia katika majukwaa ya kisiasa huku mashekhe hao na familia zao zikiendelea kupata tabu? Hapo hapo mmoja wa mashekhe hao akamwambia sheikh Saleh kua kutokana na alivo anaamin kua kama angeamua kusimama usiku na kuwaombea dua tu masheikh wale basi Masheikh wale wangepata nusra ya M/Mungu lakini inaonekana hata hilo limemshinda.

Aliendelea sheikh huyo kwa kusema kua watu waliomba dua nyingi ili kuinusuru Zanzibar na mambo mbali mbali lakini kuna viongozi wakawa wanapita na kusema kua vi Alamtara vyenu havitowasaidia chochote sasa je mtu kama huyu ambaye anadharau na kuidhalilisha hadi Quran (maneno ya Mungu) nae tushirikiane nae?

Hakika sheikh Saleh ambaye ni mufti mkuu wa Zanzibar juzi alipata wakati mgumu sana na hii imetokana na kukubali kutumiwa na CCM pamoja na ukweli kwamba ukweli na chanzo cha matatizo haya yote anajua wazi kua yamesababishwa na CCM kwa dhambi walioifanya ya kuwadhulum Wazanzibari.

CCM kwa sasa hakuna mtu anaeweza kuisadia au kuinusuru katika namna yoyote ile maana imekataa kufata maamrisho ya Allah ya kutenda haki na kuacha dhulma.

Shein anaposema kua kauli za ubaguzi na kuzigawa jamii zimekatazwa katika dini zote huku akajitia sahau kua dhulma imekatazwa zaidi ni sawa na hayo aliyoyasema sheikh kua anakoroga kinyesi halafu anategemea kuskia harufu mzuri au anataka kuyafikia mafanikio lakini hafati njia za mafanikio.

Sisi tunasema tena tutawagomea na hatutoacha kuwagomea mpaka watubu na moja ya sharti ya toba ni kama alivyosema mmoja wa masheikh hao kua ni kuirejesha haki kwa uliowadhulum.

Na hii ndio toba pekee ya CCM itakayotufanya tuache kuwagomea, pasi na kufanya hivyo tutawagomea mpaka wachanganyikiwe.

# Hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke#

Abdalla Dadi.

Tagsslider
Share: