AudioHabari

Sauti – Mzee Moyo na DW Radio

Sikuzaliwa kama nitabakia CCM miaka yote, CCM si Mama yangu si Baba yangu si Rafiki yangu, kama alivyosema Mwalimu Nyerere.
Mzee Hassan Nassor Moyo, asema hayo baada ya kuhojiwa na Souti ya Ujewumani. dw.de.

Mzee Moyo ajibu kufukuzwa kwake uwanachama wa CCM!

“Nimeiasisi CCM, kadi yangu ni namba 7. Hata hivyo kufukuzwa uwanachama sio tatizo kwa sababu CCM sio mama yangu wala sio baba yangu.

Sitobadilisha msimamo wangu wa kuitetea Zanzibar. Nimefanya hivyo tokea ASP na CCM hazijaasisiwa. Muungano na Katiba ni masuala ya Nchi sio Mali ya CCM.

CCM sijaikosoa hadharani Bali nimeieleza ukweli.

Uwamuzi wao wa kunifukuza haunishughulishi”

CCM Zanzibar yamfukuza Moyo

Chama cha Mapinduzi visiwani Zanzibar kimemvua uanachama mmoja wa waasisi wake, Mzee Hassan Nassor Moyo, ambaye mbali ya kuwahi kushikilia nyadhifa mbalimbali kwenye Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiye pia aliyeongoza Kamati ya Maridhiano miaka mitano iliyopita ambayo ilifanikiwa hatimaye kuasisi muundo wa serikali ya pamoja.

Tagsslider
Share: