Habari

Sauti:Miaka 48 ya Muungano wa Tanzania: Unaelekea wapi?

Karibuni miaka 50 baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado masuala ya msingi kuhusiana na Muungano huo bado hayajajibiwa, licha ya Tanzania kuelekea sasa kwenye Katiba Mpya.

Katika kipindi hiki cha Maoni kutoka DW Kiswahili, Othman Miraji anaongoza majadiliano na Profesa Julius Nyang’oro wa Chuo Kikuu cha North Carolina, Marekani; Hamza Hassan Juma, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CCM; mwandishi wa habari Jenerali Ulimwengu wa Dar es Salaam na mwandishi wa habari Salim Said Salim wa Zanzibar.

Kusikiliza kipindi hiki, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Play

Chanzo:DW-Swahili

Share: