Habari

Serikali haramu ya SMZ: Ndio Wanao-endelea Kuizalilisha Zanzibar na Wazanzibari.

Asalamu aleikhum Ndugu zangu wazanzibari wa Nje na Ndani ya Visiwa Vyetu Adhimu. Ama mimi sina budi ila kumshukuru Muumba wa mbigu na Ardhi (ASW) na kunijaalia kufika hapa tena na makala hii yenye kichwa cha habari hapo juu.

1. Serikali Haramu iliojiweka Madarakani:

Sio Kalamagamba au mwenziwe Kalamaganda alie izalilisha Zanzibar, bali ni Serikali haramu isiochaguliwa na Wananchi ndio inayoendelea na itakayo endelea kuidhalilisha Zanzibar na Wazanzibari. Kwanini niseme hivo?
Nasema hivo kwakuja na mifano hai ya kimaisha katika mfumo wetu sisi binaadamu. Ikiwa wewe binaadamu mwenyewe utajivunjia heshima kwa niaba yoyote ile basi hakuna mtu mwengine yoyote atakae kuheshimu. Na kibaya zaidi, unaweza ukajipotezea hata maisha na ulichonacho coote kwakuto kujiheshimu.
Na kwa upande wa nchi ya Zanzibar, Wazanzibari wenzetu akiwemo DR Ali Mohamedi Sheni na Wazanzibari wengine ambao Wanajiita Viongozi halali wa SMZ. Hawa ndio Waliotudhalilisha na Wataendelea kutudhalilisha hadi tutafika kugeuzwa kama lile kabila la ROHINJA kule BARMA. Viongozi hawa wameivunjia heshima Zanzibar na Wazanzibari siku ile ya tarehe 28.October 2015. Wakati walipoyafuta matokeo halali ya Uchaguzi huru na haki uliofanywa.
Na baadae wakatoka Watwana ambao hujiita “Wana Mapinduzi na waasisi wa Uhuru wa Muafrica” wakenda Kuomba Jeshi la TANGANYIKA kwa Jakaya Kiwete ili lije lipindiwe matokeo halali ya Uchaguzi na kuwakanusha Wazanzibari kwa mara ya 5 haki yao ya kujichagulia viongozi wanao ona kwamba wanaweza kuwaletea heshima ya Visiwa vyao.

2. Kuivunja Katiba ya Zanzibar na Maradhiano yaliopatikana 2009

Jengine lilofanywa na Wazanzibari wenzetu wa CCM ni lile la kuvunja katiba ya Zanzibar na Kuikanyaga kanyaga baadae wakaikojolea na kuipaka Mavi. Tukumbuke muafaka wa Kamati  ya  watu 8 wa CCM na CUF uliofanywa na ndugu Amani Karume na maalim Sefu 2009. Muafaka ule uliweza kuanza kuitoa Zanzibar katika siasa za visasi. Ukweli uliokuwepo nikwamba Muafaka ule haukufurahiwa na viongozi wa Serikali ya Tanganyika/ Tanzania. Na raisi aliekuweko Jakaya kikwete alilaumiwa sana na Viongozi wenzake kama vile Mkapa, Mzee Ruksa, Samuel 6 na Vidudu watu wengine Wazanzibar walijitokeza kama vile Shamsi Vuai, Vuai nk.

Kama tunavojuwa ndugu wazanzibari Muungano huimarika kuijenga Tanganyika na Kuiharibu Zanzibar kijamii na kiuchumi pale ambapo WaZanzibar hawasikilizani. hapo Tanganyika hujiimarisha kujenga nchi yao kwakutumia Ruzuku na misaada mingi inayomiminwa na wafadhili kwa jina la Muungano.

Kwahivo viongozi wa CCM Tanganyika walikua wanatafuta pahali ili waweze kuwakoroga  Wazanzibari na kuwarejesha nyuma zaidi ya miaka 50. Sababu ilipatikana baada ya CCM kukosa Kura  Zanzibar nakuungana na Wasaliti wa Kizanzibari kuivunja Katiba yao wenyewe. CCM Zanzibar kutoiuthamini Katiba ya Zanzibar  nalo limewafanya viongozi wa CCM Tanganyika  kupata njia nzuri yakuimaliza Zanzibar.

Kuna rafiki yangu ananambia wakati Baraza la wawakilishi Linapashuka na kudodosa Vipengele vya Katiba ya Tanganyika ya 1977. Baadhi ya viongozi wakuu wa Tanganyika walikua wanacheka kabisa. Nakujiuliza Kulikoni?  Hivo hawa wawakilishi wanaopayuka pale Zanzibar wanajuwa hasa ni nani alieivunjiya Heshima Zanzibar na Wazanzibari – Isee si niwao kwa wao?

Genge la Mazombi linalopayuka hapo BLW leo ndilo genge hilo liovunja katiba ya Zanzibar kwa ajili tuu ya Madaraka katika SMZ na wakasahau Consequance yake ni nini?

Matokeo yakuvunja katiba ya Zanzibar nakujiweka madarakani bila ya idhini ya Wananchi ndio imepelekea Kalamaganda Kabudi na Watanganyika Wennzake wazidi kuivuruga Jamii ya Kizanzibari.
Naamini kama Serikali hii ingeshikwa na Viongozi waliopata ridhaa ya Wazanzibari, basi tamko la kalamaganda lingekuwa ni mwiba mkali sani.

Ndugu Wazanzibari kuna mengi yakuudhi na kukera yanakuja na yameandaliwa na hao tunaowaita WWBLW pamoja na Mabwana zao CCM Tanganyika.

Usikose kusoma makala yangu ya 2. Inaendelea

Share: