Habari

Serikali yawaonya viongozi wanaodhalilisha wafanyakazi

October 1, 2018

NA MADINA ISSA

SERIKALI imesema haitosita kumchukua hatua za kinidhamu kiongozi yeyote, atakayebainika kutumia madaraka yake vibaya kwa kumrubuni mfanyakazi wake kwa kisingizio cha kumpa nafasi katika kazi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohammed Ahmada Salum, aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na virusi vya homa ya ini, kwa viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, hafla ambayo ilifanyika ofisini za Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Mazizini.

Alisema ingawa tatizo hilo sio kubwa ila kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiendeleza rushwa ya ngono sehemu za kazi, jambo ambalo halikubaliki.

Alisema baadhi ya viongozi wanatumia nafasi zao kudhalilisha wafanyakazi jambo ambalo linapaswa kukemewa.

Alisema masuala hayo yakiendelezwa, heshima katika sehemu za kazi itapungua na hivyo kuzorotesha ufanyaji kazi.

Alisema kiongozi mzuri ni yule anayesimamia wafanyakazi walio chini yake kwa kushirikiana nao vizuri katika kazi.

Zanzibarleo

Share: