HabariVidio

SHAMHUNA NI MMOJA TU KATI YA WANAOTUKAANGA WAZANZIBAR!

 

Napata mashaka kuwa mchezo alioucheza waziri Shamhuna wa kutengeneza serikali ndani ya serikali kwa mambo mazito yanayohitaji kuamuliwa na baraza la mawaziri kwa pamoja si mchezo mpya bali ni wakati tu ndio umekataza kuendelea kwa hilo, na hili linawezekana pia kuwa lipo hivi sasa tunaposema hivi! Usishangae kuna waziri mfano wa Shamhuna nae ana lake anapika lihewani bila kulihusisha baraza la mawaziri, na hata wawakilishi wetu pia si hasha hawayajui mfano wa hili, na wana sababu zao wahafidhina hawa za kuyapika wanayoamini ni maovu na wanaamini hawatafanikiwa watakapoyafikisha baraza la mawaziri, na hawa tukiwatafuta tutawakuta ni wale waliokuwa wakipita na kuzunguka Zanzibar kuwakataza waZanzibar kuukataa umoja huu tulionao sasa!
Tafakari na Zinduka Sasa Mzanzibar
Share: