Habari

Shein, UVCCM na Wenzake

Ukitathmin hali ya siasa ya Zanzibar sio shwari. Zimerudi tena zile siasa za kutupiana madongo, kibaguzi, na haileti taswira nzuri kw amnasaba wa hali ya maridhiano ya kisiasa Zanzibar. Tunakubali kuwa ‘political transition’ inakumbwa na misuko suko kama hii tunayoiona, lakini kigezo (benchmark) kubwa katika hiyo ‘political transition’ ni kubadilika tabia (attitudinal/behavioural change).

Kwa Zanzibar hii bado haijatokea: Shein na wenzake wanaishi kama vile leo ni siku ya mapinduzi ya 1964. Hebu ingieni katika vichwa vyao wanafikiri nini, kama vile mapinduzi ya 1964 yamefanyika leo, sio 2013 (21st century, chini ya kivuli cha GNU, ndani ya pressure cooker la katika mpya, kuelekea 2015 elections,kusaidia jamii hasa vijana ambao wengi hawana kazi si wale waliosoma tu, bali hata wale wasiosoma — ngoma draw.

Jana Ikulu ya Zanzibar eti imekanusha habari iliyoandikwa na Mwinyi Sadalla wa Nipashe kuhusu Shein-Karume. Mimi naona habari hii ni kweli, na huu ndio msimamo halisi wa Shein, na tumeona UVCCM msimamo wao ni kama huo. Sijui Shein na wenzake wanakanusha nini.

Imechanwa picha ya Karume pale Kisonge, na Shein, Vuai wamekaa kimya! mengi yamefanywa na kusemwa dhidi ya Karume na CCM-Karume; Shein na wenzake wamekaa kimya; UVCCM sasa imepata wahuni zaidi kuliko wakati wote tunaoujua sisi. Na Shein, na wenzake anawatizama tu.

Kuna madai kuwa UVCCM wanakusudia kufanya vurugu, fujo katika mchakato huu wa kupata katiba mpya, ikiwemo kuvamia mabaraza ya katiba ili walazamishe serikali MBILI kuelekea MOJA. Sasa, je – kama Watanganyika hawataki serikali mbili/Moja UVCCM Zanzibar mtasema nini? Na mtataka serikali ngapi, na kutoka kwa nani. Hee nyie UVCCM fumbueni mamcho, open up your minds bwana weee?

Leo UVCCM na CCM mmeandaa kongamano pale SUZA (juzi) mmetafuta watu kutoka bara wote kuja kutusemea Wazanzibari, against our will, against our consent, na matakwa yetu, na madai yetu kwa ajili ajili ya kupata nchi yetu: je, nyie Tanganyika, kwa mfano, Mtwara, mmeshapitisha uamuzi Fulani wenye maslahi kwenu – tuje sisi wazanzibari tupinge hadharani madai yetu ya halali — mtakubali? Mgeni kutoka nje ya mtaa wenu apinge maamuzi ya msingi ya umma wa waliowengi.

Dr.Shein, UVCCM na wenzako, madai ya serikali tatu hayakuanza leo wala jana. Karume Sr (alifikiria huko, na alikuwa akitamka hadharani, hotuba zake zipo ingawa sasa nasikia nyingi zimefutwa au zimeibiwa), Jumbe + Ramadhan Haji Faki walidai serikali tatu 1984, wakafukuzwa CCM na kuwekwa under house arrest; Seif Shariff na timu yake – pia walidai serikali tatu, mid 80s/wakafukuzwa na kutiwa ndani, G55 — wabunge wa Tanganyika (1993) walifanya petition kudai serikali tatu, wakapigwa na chini madai yao: tume ya Nyalali 1992/93 kwa upanda na marefu.

Marehemu Daurado aliandika paper nadhani 1984 pia ilidai serikali tatu kama sulhu ya matatizo ya muungano. Basi wewe Shein na UVCCM kweli hutaki kuona ukweli hata kama sera na ilani ya CCM ni serikali mbili kuelekea MOJA. Lakini umma wa Watanzania na Zanzibar unataka kinume na hilo. je, mtawapiga risasi, mtawafanya NINI? je, kama Tanganyika ‘point blank’ watasema wote wanataka serikali tatu, na hususan wanataka Tanganyika yao, utawafanya nini (Dr.Shein — kumbuka kuwa you can not turn the clock back……! imefika saa sita, ndio saa sita haiwezi tena kurudi saa tatno au nne). Balahau weee, amka balahau — amiiiiii!Wewe Dr.Shein umewasahau jamaa zako wale -Al Maashiri!!
l

Share: