Habari

Sherehe za Uhuru wa Zanzibar December 10

Nikiizungumzia Zanzibar utambulisho wake ni Uhuru wa December 10 1063. Nchi iliyokuwa chini ya himaya ya Malkia wa Uingereza kama vile zilivyokuwa nchi nyengine kama vile Australia, Canada, na nyenginezo.

Uhuru wa December 1o ni utambulisho wa Zanzibar kama dola huru lenye watu wake, mipaka yake, katiba na mamlaka zake. Ndio siku hii inayotambulika kitaifa na kimataifa. Kuisahau siku ya december 10 ndio kuifuta Zanzibar katika ramani ya dunia.

Isifike huko kwani Zanzibar ipo na Wazanzibar pia wapo. Hivyo basi waendelee kuienzi kama ndio siku muhimu ya Wazanzibar mbele ya uso wa dunia, kitaifa na kimataifa.

Vizazi viendelee kurithishwa umuhimu wa kuitambua na kuikumbuka kwani sio tu kuihuisha dola ya Zanzibar bali pia kutunza na kuendeleza historia sahihi nchi yetu iliyopitia. Huwezi kufika kileleni kama hujapitia shinani.

Share: