HabariVifo

Shk.Nassor Bachu amefariki

Inna lillahi wa inna ilaihi rajiun!

Kwa taarifa za kuaminika hii leo zinaeleza kuwa sheikh Nassor Bachu amefariki hii leo. Sheikh alianza kuugua ghafla kwa kupata stroke na baadaye kuendelea kujiuguza nyumbani kwake huku akizuiwa kudarsisha chochote kutokana na hali yake kiafya. Kwa kipindi cha kama mwaka hivi hali yake ilizidi kuwa mbaya na kubakia kuuguzwa kitandani tu na hivyo akapelekwa India mwishoni mwa mwaka 2012 kwa matibabu na kuelezewa kuwa ana mgando wa damu ndani ya ubongo wake. Tiba haikuwepo kwa hali hiyo na hivyo kurejeshwa nchini na kuendelea na dawa za kawaida.

Sheikh aliwahi kuzushiwa kifo sio chini ya mara tatu na kusababisha mwanawe kuanza kutoa taarifa katika vyombo vya habari ikiwemo redio imani kuwa ni habari za uzushi na wala familia haijapata kuomba msaada wa mchango wa matibabu.

Maziko yatakuwa kesho (14/02/2013) saa nne asubuhi Chukwani (wanawake), kusaliwa ni Masjid Sunna Kikwajuni na kuzikwa Donge – Unguja  inshallah.

MOLA AMSAMEHE MADHAMBI YAKE, AMJAALIE KAULU THABIT NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.

Tagsslider
Share: