Habari-Picha

Ni mbili, tatu utapigwa tuu!

Wengi tunashangazwa na mwenendo wa viongozi wa juu wa serekali ya CCM.Kiilivyo mchakato huu wa katiba hatua iliopo sasa ni kuandika katiba mpya au kupitisha ikawa sheria ya nchi.

Kinachojitokeza sasa ni mijadala ambayo inachochewa na viongozi wa juu kwa kuibua mijadala na maoni ambayo muda wake haswa umeshapita.Maana sasa hivi sio hatua ya kukusanya maoni, ni kupitisha au kuboresha rasimu ili katiba au sheria.

Badala ya kumsikia Mh.Pinda akilazimisha serekali mbili, imenijia tena ile kauli yake ya kuhalilisha kipigo kupitia jeshi la polisi.Haijatofautiana sana hii ya serekali mbili.

Nashauri wananchi wakaanza kujipanga visiwani Zanzibar kwa kampeni za nyumba hadi nyumba kuikataa katiba endapo haitaleta mabadiliko yoyote katika mfumo wa muungano.

Wasalaam

Tagsslider
Share: